TIMU
ya AS FAR Rabat ya Morocco itakayoikabili Azam kwenye mechi ya Kombe la
Shirikisho inatua nchini leo (Aprili 17 mwaka huu) saa 7.30 mchana kwa
ndege ya Qatar Airways.
Msafara
wa timu hiyo wenye watu 28 kwa ajili ya mechi hiyo ya kwanza ya raundi
ya pili itakayochezwa Jumamosi (Aprili 20 mwaka huu) saa 10 kamili jioni
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam utafikia hoteli ya Sapphire iliyoko
maeneo ya Kariakoo.
Wakati
Azam imetinga hatua hiyo baada ya kuitoa timu ya Barrack Young
Controllers II ya Liberia kwa jumla ya mabao 2-1, AS FAR Rabat imeingia
raundi hiyo moja kwa moja kutokana na nchi hiyo kufanya vizuri kwenye
michuano ya klabu Afrika.
Timu
nyingine ambazo zimeingia raundi hiyo moja kwa moja katika Kombe la
Shirikisho kama ilivyo AS FAR Rabat ni Asec Mimosas ya Ivory Coast,
Atletico Petroleos (Angola), C.S.S. (Tunisia), DC Motema Pembe (Jamhuri
ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), El Ahly Shandy (Sudan), Enppi (Misri),
Heartland (Nigeria), Ismaily (Misri), Lobi Stars (Nigeria), U.S.M. Alger
ya Algeria na Wydad Casablanca (Morocco).
Mwamuzi
Emile Fred atakayesaidiwa na Steve Maire, Jean Ernesta na Jean Claude
Labrossa wote kutoka Shelisheli ndiye atakayechezesha mechi hiyo.
Kamishna ni Abbas Sendyowa kutoka Uganda. Waamuzi watawasili nchini
kesho (Aprili 18 mwaka huu) jioni.
MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI
Ujumbe
wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambao uko nchini
kwa ajili ya kushughulikia mchakato wa uchaguzi mkuu wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utakutana na waandishi wa habari leo
(Aprili 17 mwaka huu) saa 10 jioni hoteli ya Serena.
Mkuu
wa Idara ya Uanachama ya FIFA, Primo Covarro ndiye aliyeongoza ujumbe
huo ambao una siku tatu tangu ulipowasili nchini kushughulikia suala
hilo.
Ujumbe
huo jana (Aprili 16 mwaka huu) ulikutana na Sekretarieti ya TFF, Kamati
ya Uchaguzi ya TFF, wagombea ambao walikata rufani FIFA na ambao
waliomba marejeo (review) ya rufani zao kwa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi
ya TFF.
Leo asubuhi ujumbe huo wa FIFA ulitarajiwa kukutana na Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF inayoongozwa na Idd Mtiginjola.
0 maoni:
Post a Comment