Rais Ngowi akiwa amesimama na Mkurugenzi
Mtendaji wa BNSC bwana Persy Raditladi
rais Ngowi akihutubia katika miytano wa
waandishi wa habari katika ukumbi wa
BNSC
Rais Ngowi yuko nchini Botswana kuutangaza mkanda wa ubingwa wa ngumi wa kimataifa ambao utashindaniwa tarehe 5 July nchini Namibia kati ya bondia wa Botswana Lesley Sekotswe na bondia kutoka Namibia Immanuel Naidjala. Wawili hao walitoka sare katika mpambano wa kukata na shoka wa kugombania mkanda huo tarehe 20 Machi mwaka huu katika jiji la Windhoek, nchini Namibia.
Serikali ya Botswana imeahidi kufanya kila liwezekanalo
kuhakikisha kuwa programu ya “Utalii wa Micheazo ya IBF” inanufaisha nchi hii
yenye vivutio kadhaa vya kitalii likiwamo bonde la maarufu la “Okavango Delta”
Katika mazungumzo yao Rais Ngowi alieleza jinsi IBF
inavyozinufaisha nchi ambazo zimeingia katika programu hii na namna mabondia
wanaotoka katika nchi hizi wanavyonufaika na viwango vya kimataifa vya IBF.
Ngowi aliielezea Botswana kama nchi yenye neema ya vipaji vya mabondia wazuri
wa ridhaa na kuwashauri kuwa waweke mikakati ya mabondia wa ridhaa wanavyoweza
kujiunga na ngumni za kulipwa ili waweze kufaika na vipaji vyao.
Nchi ya Botswana ni moja kati ya nchi zenye mabondia wazuri
katika ngumi za ridhaa lakini kumekuweko na pengo la kuwaendeleza wanapofikia
kustaafu na kutokuwa na uwazi wa namna ya kujiunga na ngumi za kulipwa. Ujio wa
Rais wa IBF Afrika nchini Botswana umefanyika wakati nchi hii inapokabiliwa na
sintofahamu juu ya kuwaendeleza mabondia wake wanapostaafu ngumi za ridhaa.
Mazungumzo ya Rais Ngowi na serikali ya Botswana
yalitanguliwa na mkutano wa waandishi wa habari pamoja na wadau kadhaa wa ngumi
za kulipwa uliofanyika katika ukumbi wa BNSC jijini Gaborone Botswana leo.
Katika mkutano huo Rasi Ngowi aliuonyesha mkanda wa IBF wa kimataifa katika
uzito wa bantam utakaoshindaniwa kati ya bondia wa Botswana Lesley Sekotswe na
bondia kutoka Namibia Immanuel Naidjala tarehe 5 July mwaka huu jijini
Windhoek, Namibia.
Rais Ngowi aliwahakikishia wadau wa ngumi wa Botswana kuwa IBF
itafanya kila liwezalo kuhakikisha kuwa Botswana imejenga msingi mzuri wa ngumi
za kulipwa na kutumia vipaji vilivyonavyo katika ngumi za ridhaa. Rais Ngowi
aliondoka leo kwenda nchini Afrika ya Kusini ambako atakutana na wadau wa ngumi
na kutangaza mapambano kadhaa ya IBF yanayotarajiwa kufanyika nchini humo
kuanzia mwezi ujao!
0 maoni:
Post a Comment