Mtanzania
Onesmo Ngowi ambaye ndiye ni Rais wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa katika
bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, ataongoza ujumbe
mzito kutoka bara la Afrika na Ghuba ya Uajemi kwenye mkutano wa 30 wa Shirikisho
la Ngumi la Kimataifa na Chama Cha Ngumi Cha Marekani (IBF/USBA).
Mkutano huo utafanyika
katika hotel ya nyota tano ya Concorde Berlin iliyo karibu na Kanisa la kumbukumbu la
Kaiser Wilhelm pamoja na taasisi ya Helmut
Newton na Jumba la ukumbusho wa Picha jinini Berlin, Ujerumani.
Ujumbe atakaoongoza
Ngowi utajumuisha wajumbe kutoka katika nchi za Afrika, Ghuba ya Uajemi na
Mashariki ya Kati na mpaka sasa ni nchi 31
zitakazo jumuika katika ujumbe huo ambao utajumuisha viongozi wa mashirika
mbalimbali ya kusimamia utalii, biashara na michezo.
Mbali na kuhudhuria
mkutano huo utakaofanyika kwa siku sita kuanzia Mei 21 mpaka Mei 26, ujumbe wa Ngowi utafanya pia mazungumzo na
viongozi pamoja na taasisi mbalimbali zinazosimamia Utalii, Uwekezaji pamoja
na Utalii wa Michezo katika nchi ya Ujerumani na nchi nyingine za Ulaya
ambazo zitatembelewa na ujumbe huo.
Katika msafara huo ambao
utajumuisha pia viongozi wa bodi za Utalii na Michezo kutoka katika
nchi za Botswana, Afrika ya Kusini, Ghana, Misri na Falme za nchi za Kiarabu
(UAE),ujumbe huo utatembelea pia nchi za Ufaransa, Ubeljiji, Uhispania
pamoja na Uholanzi!
Ngowi amewahimiza
watanzania juu kuchangamkia fursa za kujitangaza kibiashara nje ya nchi na
kuwataka kujituma. “Ni
muhimu Watanzania wakafungua macho na wajue kuwa dunia sasa ni kijiji na
wasipoangalia watajikuta wanabaki nyuma kila mara” aliema Ngowi ambaye kwa ujumla alionyeha
kusikitishwa na muitikio mdogo wa watanzania kwenye masuala ya kujitangaza
kibishara nje ya nchi.
Ujumbe wa Ngowi
utaondoka barani Afrika tarehe 17 Mwezi Mei na kuelekea Dubai ambako ndipo
wajumbe wote watakapokutana tayari kwa msafara wa kuelekea jijini Berlin, Ujerumani!
0 maoni:
Post a Comment