Mabondia Mwaite juma,cosmas kibuga na shabani kaoneka ni baadhi ya
mabondia wa dar es salaam watakaokwenda chalinze kuhamasisha ngumi za
kulipwa wilayani humo kwa kuzipiga na mabondia wakali wa chalize.
Kampuni inayoandaa mapambano kwa ajili ya kunyanyua vipaji vya
mabondia machipukizi ya Bigright Promotion, imaeandaa pambano hilo ili
kutanua wigo wa michezo nchini kwa kuanzia kutembelea wilaya
zinazohamasika kimchezo ikiwemo chalinze.
Tumeamua kufanya chalinze kwa sababu tunataka chalinze iwe ndio
mfano kwa kuandaa pambano hili ambalo litawakutanisha chipukizi wakali
wa dar na wakali wa chalinze,pia kutakuwepo na mapambano mengine yenye
ushindani wa hali ya juu na vituko kama vile la Pius puto atakaezipiga
na iddi mkatatiketi -hawa ni mbabe wa sokoni na mbabe wa stendi
watazipiga kumaliza ubishi wao uliotanda kwa muda mrefu. ukiondoa
pambano hilo Minyusi abdala atazipiga na shaban kaoneka, Baraka
nuhu"chalinze hamjambo" atazipiga na goodluck suleiman, alex kdo
atazipiga na herman shekivuli, iddi mwera atazipiga na ramadhan misugwa
na mapambano mengineyo mengi likiwemo la ustadh mwenye msimamo mkali
ustadh Kurasheni aliyeahidi kuchinja kama anachinja kondoo ulingoni
atakaezipiga na makali wa bodaboda mzee kachacha.mgeni rasmi wa pambano
hilo atakuwa ni diwani wa Chalinze bwilingu bw naser Karama ambaye muda
wote amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha vijana kushiriki michezo na
ametoa basi kubwa kwa ajili ya mashabikitoka daresslaam kwenda
kushangilia na kurudi.
wakati huohuo diwani Karama anategemea kujenga ukumbi mkubwa
wangumi hapo chalinze, hivyo ngumi zote za kimataifa zitakuwa zikipigwa
hapo
0 maoni:
Post a Comment