Shrikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko za kifo cha
Mkuu wa zamani wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Makame
Rashid kilichotokea juzi (Aprili 14 mwaka huu) kutokana na maradhi
jijini Dar es Salaam.
Rais
wa TFF, Leodegar Tenga amesema msiba huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira
wa miguu kutokana na mchango aliotoa Meja Jenerali Makame Rashid ikiwemo
kuwa mlezi wa timu ya Ruvu Stars wakati huo akiwa Kamanda (CO) wa
Kikosi cha Ruvu JKT.
Pia
aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mdhamini
(Trustee) wa TFF wakati huo ikiitwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania
(FAT) na wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya katika miaka ya themanini
alikuwa sehemu ya mafanikio kwa timu ya Tukuyu Stars ya Mbeya iliyotwaa
ubingwa wa Tanzania Bara mwaka 1987 ikiwa ndiyo kwanza imepanda kucheza
Ligi Kuu wakati huo ikiitwa Ligi Daraja la Kwanza.
TFF
inatoa pole kwa familia ya marehemu Meja Jenerali Makame Rashid, Jeshi
la Kujenga Taifa (JKT), Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Kamati ya
Olimpiki Tanzania (TOC), na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika
kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Maziko
yanatarajiwa kufanyika leo (Aprili 16 mwaka huu) nyumbani kwao mkoani
Mtwara. Mungu aiweke roho ya marehemu Sembwana mahali pema peponi. Amina
VPL KUTIMUA VUMBI VIWANJA VITATU
Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho
(Aprili 17 mwaka huu) kwenye viwanja vitatu huku vinara wa ligi hiyo
Yanga wakifukuzia ubingwa huo jijini Tanga.
Yanga
inayoongoza ligi ikiwa na pointi 52 itakuwa mgeni wa Mgambo Shooting
katika mechi itakayochezeshwa na mwamuzi Athuman Lazi kutoka Morogoro
kwenye Uwanja wa Mkwakwani. Waamuzi wasaidizi wa mechi hiyo ni Michael
Mkongwa wa Iringa na Godfrey Kihwili wa Arusha wakati Kamishna wa mechi
hiyo ni Godbless Kimaro kutoka Moshi.
Kagera
Sugar na Toto Africans zitaumana kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba
katika mechi namba 164 itakayokuwa chini ya mwamuzi Martin Saanya wa
Morogoro.
Uwanja
wa Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro, na wenye uwezo wa kuchukua
watazamaji 4,000 utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mtibwa Sugar yenye
pointi 33 na Oljoro JKT yenye pointi 28.
Israel
Nkongo kutoka Dar es Salaam ndiye atakayechezesha mechi hiyo akisaidiwa
na Hamis Chang’walu (Dar es Salaam) na John Kanyenye (Mbeya). Kamishna
wa mechi hiyo ni Ramadhan Mahano kutoka Iringa.
AS FAR KUWASILI KESHO KUIKABILI AZAM
Wapinzani
wa Azam katika michuano ya Kombe la Shirikisho, AS FAR Rabat ya Morocco
wanatarajiwa kutua nchini kesho (Aprili 17 mwaka huu) saa 7 mchana kwa
ndege ya Emirates.
Msafara
wa timu hiyo wenye watu 28 utafikia hoteli ya Sapphire iliyoko maeneo
ya Kariakoo, Dar es Salaam tayari kwa mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya
pili itakayochezwa Jumamosi (Aprili 20 mwaka huu) saa 10 kamili jioni
Uwanja wa Taifa.
0 maoni:
Post a Comment