Mechi
ya kwanza ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho kati ya Azam na AS
FAR Rabat ya Morocco iliyochezwa juzi (Aprili 20 mwaka huu) imeingiza
sh. 50,850,000.
Fedha
hizo katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na
kumalizika kwa timu hizo kutoka suluhu zimetokana na watazamaji 8,268
waliokata tiketi.
Viingilio
vilikuwa sh. 5,000, sh. 10,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na
sh. 30,000 ambacho kilikuwa kiingilio cha juu kwa jukwaa la VIP A.
Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo
walikuwa 7,354.
Mgawo
ulikuwa kama ifuatavyo; gharama za tiketi sh. 5,575,500, asilimia 15 ya
uwanja sh. 6,791,175, asilimia 10 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh.
4,527,450 na asilimia 75 iliyokwenda kwa klabu ya Azam ni sh.
33,955,875.
Mechi iliyopita ya Azam katika michuano hiyo dhidi ya
Barrack Young Controllers II ya Liberia iliingiza sh. 44,229,000
kutokana na watazamaji 17,128 waliokata tiketi. Viingilio vilikuwa sh.
2,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 20,000 ambacho kilikuwa kiingilio
cha juu kwa jukwaa la VIP A.
MECHI YA JKT RUVU, YANGA YAINGIZA MIL 66/-
Mechi
ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya JKT Ruvu na Yanga iliyochezwa jana
(Aprili 21 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh.
66,568,000 kutokana na watazamaji 11,864.
Viingilio
katika mechi hiyo namba 106 iliyomalizika kwa Yanga kutoa dozi ya 3-0
kwa wenyeji wao vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000
huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 15,702,752.45 wakati Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 10,154,440.68.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,984,450.40,
tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 4,790,670.24, Kamati ya Ligi
sh. 4,790,670.24, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
2,395,335.12, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh.
931,519.21 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh.
931,519.21.
0 maoni:
Post a Comment