YANGA imejiweka katika wakati mgumu wa kutwaa ubingwa wa
Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kuambulia sare ya bao 1-1 dhidi ya Mgambo Shooting
kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani, Tanga, leo.
Kwa matokeo hayo, timu hiyo imefikisha pointi 53, hivyo
kulazimika kusubiri matokeo ya mechi zake mbili zijazo dhidi ya JKT Ruvu na
Coastal Union kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam,
kuona kama itashinda zote na kuwapoka kombe
watani wao wa jadi, Simba.
Hata kama Yanga itashinda Jumapili dhidi ya JKT Ruvu, bado
ushindi huo hautawahakikishia ubingwa kwani watakuwa wamefikisha pointi 56
ambazo zinaweza kufikiwa na Azam wenye pointi 47, iwapo watashinda mechi zao
zote tatu zilizobaki.
Hivyo, ili Yanga waweze kutwaa ubingwa kabla ya mchezo wao
wa mwisho dhidi ya Simba Mei 18, watalazimika kuzifunga JKT Ruvu na Coastal Union, kitendo ambacho si rahisi kutokana na ugumu wa
wapinzani wao hao.
0 maoni:
Post a Comment