Bodi ya klabu ya MANCHESTER UNITED imempitisha kwa
kauli moja kocha wa EVERTON DAVID MOYES kuwa kocha wa MANCHESTER UNITED kwa
kuumpa mkataba wa miaka sita na ataanza kazi rasmi JULAI mosi.mwaka huu
Uteuzi huo umekuja baada ya SIR ALEX FERGUSON
kutangaza kustaafu kazi ya ukocha mwishoni mwa mwezi huu .
DAVID MOYES amesema ni heshima kubwa kuteuliwa
kufundisha timu kubwa ya MANCHESTER
UNITED amemshukuru FERGASON kwani yeye ndiye alipendekeza jina lake.
Kocha MOYEZII atatambulishwa rasmi katika klabu ya
MANCHESTER UNITED mara baada ya kumaliza mkataba wake na EVERTON JUNE 30
mwaka huu.
Moyez alianza kazi ya Umeneja Preston
North End Januari 1998 Klabu ikiwa taabani Divisheni ya Pili na ikiwa hatarini kuporomoshwa
Daraja.
Lakini Moyes, ambae alianza kuchukua
Mafunzo ya Ukocha na kupata Beji zake tangu akiwa na Miaka 22 wakati akiwa
Mchezaji, aliinusuru Preston kushushwa Daraja na Msimu uliofuata aliiwezeshe
kutinga Mechi za Mchujo za kupandishwa Daraja lakini hawakufanikiwa.
Msimu uliofuata Moyes aliifanikisha
Preston North End kutwaa Ubingwa wa Divisheni ya Pili na kupanda Daraja kuingia
Divisheni ya Kwanza ambako Mwaka 2001 aliifikisha Mechi za Mchujo za
kupandishwa Daraja lakini hawakufanikiwa.
Moyez alihama Preston na kwenda Everton
Mwezi Machi 2002.





0 maoni:
Post a Comment