Diwani wa
Kata ya Kitanzini Manispaa ya Iringa Mjini,Jescar Msambatavangu (wapili
kushoto) akimkabidhi Kikombe nahodha wa timu ya Chuo Kikuu cha Ruaha, Said
Mohamed mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari
Lager Higher Learning Pool Competition 2013 yaliyomalizika mwishoni mwa wiki Mkoani
Iringa.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo na Meneja wa
Kampuni ya Bia wa kanda za juu Kusini ,Raymond Degera.
CHUO kikuu cha
Ruaha (Rucco), juzi kilifanikiwa kutetea ubingwa wake wa mashindano ya mchezo
wa pool kwa wanafunzi wa elimu ya juu mkoani ya 'Safari Lager Higher Learning
Competition 2013' baada ya kuibuka na
ushindi wa magoli 13-10 dhidi ya chuo kikuu cha Mkwawa katika mchezo wa fainali
ya mashindano hayo.
Mashindano hayo
yaliyoshirikisha vyuo vikuu vitatu vya mkoani hapa yanayodhaminiwa na Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL) yalifanyikia kwenye ukumbi wa Twisters.
Chuo kikuu cha Ruaha
kwa kutwaa ubingwa wa mkoa huo kwa wanafunzi wa elimu juu mkoani hapa mbali ya
kujinyakulia fedha taslim Sh.500,000 pia kilikata tiketi ya kuuwakilisha mkoa
huo katika fainali za taifa za mashindano hayo zitakazofanyika kuanzia Juni
mosi mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Nafasi ya tatu ya
mashindano hayo ilichukuliwa na chuo cha Tumaini ambacho kilizawadiwa fedha
taslim Sh.300,000.
Mbali ya vyuo hivyo
kupata fedha hizo taslim lakini pia kila chuo kilipata mbuzi mmoja mmoja
waliotolewa na diwani wa kata ya Kitanzini katika manispaa ya Iringa mjini,
Jesca Msambatavangu ambaye ndiye aliyekuwa mgeni mgeni rasmi katika kilele cha
mashindano hayo.
Kwa upande wa
mchezaji mmoja mmoja (wanaume), Said Mohamed wa chuo cha Ruaha alifanikiwa
kutetea ubingwa wake baada ya kumfunga Hamphrey
Tengie wa chuo cha Tumaini magoli 3-0.
Mohamed kwa kutwaa
ubingwa huo alizawadiwa Sh.150,000 na pia kukata tiketi ya kuuwakilisha mkoa
huo katika mashindano hayo ngazi ya fainali wakati, Tengie alliyeshika nafasi
ya pili alizawadiwa Sh.100,000.
Na kwa upande wa
mchezaji mmoja mmoja (wanawake), Hellen Kitali wa chuo cha Tumaini alitwaa
ubingwa huo baada ya kumfunga Beatrice Nadafu wa chuo cha Ruaha magoli 4-3 na
kujinyakulia Sh.100,000 na tiketi ya kuuwakilisha mkoa huu katika fainali za taifa, wakati Beatrice
aliyeshika nafasi ya pili aliondoka na Sh.50,000.
Zawadi zote kwa
washindi zilikabidhiwa na diwani wa kata ya Kitanzini, Jesca Msambatavangu
ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi.
Baada ya kukabidhi
zawadi kwa washindi, diwani huyo licha ya kuwapongeza mabingwa wa mashindano
hayo pia aliwataka wachezaji wa vyuo vingine ambao hawakuchukuwa ubingwa
kuongeza bidii ya mazoezi ili mwakani waweze kufanya vizuri.
0 maoni:
Post a Comment