Mwenyekiti wa UN Tanzania Human Rights Group Bw. Tobias Rahm akitoa mada kuhusu haki za binadamu jinsia na mitazamo ya Mataifa Mbalimbali ulimwenguni kuhusu Uhuru wa Habari na Haki za Binadamu siku ya mwisho ya Kongamano la maadhimisho ya Uhuru wa Habari duniani kwenye Hoteli ya Naura Springs jijini Arusha. (Picha na Dewji Blog).
Mkurugenzi wa Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene akitoa maoni yake katika kuchangia Azimio la Arusha la kupaza sauti za waandishi wa habari kudai uhuru wa habari kwenye siku ya pili ya kongamano la kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Habari Duniani lililomalizika leo jijini Arusha.
Pichani juu na chini ni washiriki wa kongamano la siku mbili la kuadhimisha siku ya uhuru wa habari duniani hapa wakiwa wanafuatilia mjadala na mada mbali mbali zilizopelekea kutoka na azimio la Arusha la waandishi wa habari katika kudai mambo mbali mbali zikiwemo changamoto na sheria za tasnia hiyo zinazotumika hapa nchini.
Mwakilishi wa COMNETU ya nchini Uganda Jimmy Okello akitoa mada kwenye kongamano hilo juu ya Usalama na Ulinzi wa waandishi wa habari wa Kenya na Uganda na kueleza kuwa hali Usalama na Ulinzi kwa waandishi wa habari kwenye nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zinalingana hazitofautiani japo zingine zimepiga hatua kwa sheria ya uandishi wa habari kuingizwa kwenye Katiba.
Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha Nyirembe Munasa, Mwenyekiti wa UN Tanzania Human Rights Group Bw. Tobias Rahm na Mwenyekiti wa UNCG Yusuph Al Amin kutoka UNESCO wakifuatilia mada mbali mbali zilizokuwa zikijadiliwa ambapo leo waandishi wa habari wametoka na Azimio la Arusha linalohusu mazingira ya usalama wao wawapo kazini na mazingira ya vyombo vya habari ikiwemo pia Serikali.
Mwalimu Ayubu Rioba akifuatilia kwa umakini mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye kongamano hilo.
Mama Rose Haji wa UNESCO wakifurahia jambo Operations Manager wa Mo Blog Zainul Mzige.
Mwakilishi wa Mo Blog jijini Arusha Mahmoud Ahmed (kushoto) akiwa na mhariri wa Sibuka Fm Felix Kaombwe wakifuatilia majadiliano mbali mbali yaliyozua Azimio la Arusha la Uhuru wa Habari ikiwemo kupitishwa kwa sheria ya Uhuru wa Habari kwenye Katiba yetu na masuala ya Usalama wa mazingira katika kazi zao za kila siku.
Usia Nkhoma Ledama wa UNIC akiteta jambo na Mwenyekiti wa UN Tanzania Human Rights Group Bw. Tobias Rahm wakati wa Kongamano la siku mbili lillilomalizika leo jijini Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Nyirembe Munasa akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magessa Mulongo wakati wa kufunga kongamano la Uhuru wa Habari Duniani lililomalizika leo jioni jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara ambapo amewaasa wanahabari kutimiza majukuma yao na kutoiyona Serikali kuwa inayafumbia macho madai yao na kuwa Azimio waliolotoka nalo litafanyiwa kazi ili kuboresha muhimili wa tasnia hiyo.
Mwenyekiti wa UNCG Yusuph Al Amin kutoka UNESCO akiongea kwa niaba ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofanya kazi hapa nchini na kutoa shukrani kwa kuona ushiriki na kufana kwa hafla nzima ya Kongamano la Uhuru wa Habari Duniani na kuwa na imani kwamba Azimio la Arusha la Wanahabari litafanikiwa. Kongamano hilo limemalizika leo jioni kwenye Hoteli ya Naura Springs jijini Arusha.
Mkongwe wa Habari Mama Eda Sanga (mwenye sweta jeupe) akiwa na wanafunzi wake wakibadilishana mawazo mwishoni mwa Kongamano la Uhuru wa Habari Duniani. Kulia kwake ni Gladness Munuo na Wa pili kulia Cecilia Mng'ong'o na Aliyekaa ni Dominica Haule wote ni wafanyakazi wa GEMSAT.
Mmoja wa waandishi wa siku nyingi kwenye tasnia ya habari ambaye pia ni Mwanaharakati wa kutetea haki za Wanawake Bi. Leila Sheikh akiwa na Mhariri wa Sibuka Fm Felix Kaombwe na Meneja wa Program za Vipindi wa Mpanda Fm Bw. Revocutus Andrew nje ya ukumbi wa mikutano.
0 maoni:
Post a Comment