Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limelitaka Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) kuanza upya mchakato wa uchaguzi baada ya kubaini
kasoro iliyotokana na ukosefu wa kutokuwepo vyombo vya kushughulikia
ukiukwaji wa maadili.
FIFA
ambayo ilituma ujumbe wake katikati ya mwezi uliopita kufanya utafiti
kuhusu mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa TFF ambao ulisimamishwa baada ya
baadhi ya wagombea kulalamika, imetaka uchaguzi ufanyike kabla ya tarehe
30 Oktoba 2013, lakini ukitanguliwa na mabadiliko ya katiba ambayo
yatahusisha uundwaji wa vyombo vya kushughulikia ukiukwaji wa maadili.
Raiswa
TFF, Leodegar Tenga aliwaambia waandishi wa habari kwenye ukumbi wa
mikutano wa shirikisho hilo kuwa suala la Tanzania lilijadiliwa kwenye
kikao cha Kamati ya Dharura ya FIFA kilichofanyika tarehe 28 Aprili 2013
na maamuzi yake kutumwa juzi kwa barua iliyosainiwa na KatibuMkuuwa
FIFA, Jerome Valcke.
Baada
ya kupokea barua hiyo, Rais wa TFF alifunga safari kwenda Dodoma jana
kukutana na Mheshimiwa Waziri na Naibu wake pamoja na Mwenyekiti wa
Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
“Matarajio
yetu sote yalikuwa kupokea majina ya waliopitishwa ili tufanye
uchaguzi. Kinyume chake tumepokea maagizo hayo. Hata hivyo tumeona kuwa
hili ni jambo la kheri kwa vile siyo tu haki itatendeka bali pia
itaonekana imetendeka.” alisema Tenga, ambaye alishatangaza kuwa
hatagombea tena urais baada ya kuliongoza Shirikisho kwa vipindi viwili
vya miaka minne kila kimoja.
“Lengo
letu ni kuhakikisha maagizo hayo yanatekelezwa na uchaguzi kufanyika
mapema iwezekanvyo kabla ya tarehe iliyotolewa. Yale mambo nayoweza
kufanyika kwa pamoja yatafanyika ili tuharakishe utekelezaji wa maagizo
yaliyotolewa na FIFA.”
Uchaguzi
wa TFF ulipangwa kufanyik tarehe 23 na 24 Februari 2013 na ulikuwa
ukielekea ukingoni, lakini baadhi ya wagombea walienguliwa katika hatua
ya mwisho na Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF na ndipo walipo andika
barua FIFA kuomba iingilie kati.
Rais
Tenga alisema kuwa ujumbe wa FIFA ulikutana na pande zote
zilizoathiriwa na mchakato wa uchaguzi na kwamba baada ya kukusanya
taarifa hizo, maagizohayo ya FIFA sasa yatakuwa ni suluhisho la matatizo
ya muda mrefu katika uendeshaji wa mpira wa miguu nchini.
Katika barua hiyo, FIFA imeiagizaTFF:
1. Kuunda
vyombo sahihi (Kamati ya Maadili itakayokuwa na vyombo viwili ambavyo
ni cha kutoa maamuzi ya awali na cha rufaa) ambavyo mamlaka yake
yatakuwa ni kushughulikia masuala ya ukiukwaji wa maadili;
2. Kufanya mabadiliko ya katiba kwa kuzingatia uundwaji wa vyombo hivyo;
3. Kuanza
upya kwa mchakato wa uchaguzi wa Kamati ya Utendaji kwa kufungua
milango kwa wagombea ambao walishachukua fomu na wagombea wapya:
4. Shughuli hiyo ikamilike ifikapo tarehe 30 Oktoba 2013.
Katika
kutekeleza hayo, TFF inatakiwa iitishe Mkutano Mkuu wa Dharura kwa
ajili ya kufanya mabadiliko ya Katiba kwa ajili ya kuunda kamati hizo za
maadili na Kanuni za Uchaguzi kabla ya kuendelea na Mkutano Mkuu wa
Uchaguzi wa Kamati Mpya ya Utendaji.
Katika
maoni yake FIFA imeeleza kuwa katika mchakato, Kamati ya Uchaguzi ya
TFF iliwaengua au kupitisha baadhi ya wagombea kwa kubaini kuwa
walikiuka Ibara ya 9 (7) ya Kanuni za Uchaguzi na pia Ibaray a 29 (7) ya
Katiba ya TFF ambavyo vinahusisha suala la kufungua kesi mahakamani,
kufuja fedha za shirikisho na ukosefu wa uwajibikaji wa pamoja.
Hata
hivyo, FIFA ilisema kuwa watu hao walitakiwa waadhibiwe kwanza na
kamati husika (kamati za maadili) kabla ya kuenguliwa na kamati za
uchaguzi za TFF.
“Kutokana
na ukosefu wa kamati za maadili matokeo yake, mmoja wa wagombea amekuwa
akienguliwa kwenye uchaguzi kila anapombea bila ya kujua adhabu yake ni
ya muda gani,” inasema barua hiyo ya FIFA.
Rais
Tenga ameagiza kuitishwa kwa kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji
ya TFF kupokea maagizo ya FIFA na kupanga ratiba ya utekelezaji wake kwa
lengo la kuhakikisha kuwa mchakato huu unatekelezwa mapema
iwezekanavyo.
0 maoni:
Post a Comment