Thursday, May 30, 2013

MARK HUGHER AWA KOCHA WA STOKE CITY KWA MIEZI SITA

Baada ya kutimuliwa na klabu ya QPR kocha MARK HUGHES sasa amechakuliwa kukinoa kikosi cha STOKE CITY kwa muda wa miezi sita.

HUGHES amechukua nafasi ya aliyekuwa kocha wa STOKE CITY  TONY PULIS, ambaye alitimuliwa na timu hiyo wiki iliyopita baada ya kuifundisha kwa muda wa miaka saba.

MARK HUGHES, mwenye umri wa Miaka 49 na ambae aliwahi kuzichezea Klabu za Manchester United, Barcelona na Chelsea, alitimuliwa QPR Mwezi Novemba Mwaka jana.

Hughes alianza kazi ya Umeneja Mwaka 1999 akiwa na Timu ya Taifa ya Wales kisha Blackburn Rovers Mwaka 1994 na baada Miaka minne kuhamia Manchester City ambako alidumu Miezi 18 na kubadilishwa na Roberto Mancini.

Baadae akaenda Fulham alipokaa Msimu mmoja na kuhamia QPR Januari 2012 na kuinusuru kushushwa Daraja lakini Msimu uliofuatia, ule wa 2012/13, Miezi mitatu tu tangu uanze, akafukuzwa.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU