MAZOEZI kwa ajili ya kujiandaa na shindano la kumsaka malkia wa Mkoa wa Tanga mwaka huu Redd's Miss Tanga 2013" yanaanza leo kwenye Ukumbi wa Lavida uliopo jijini Tanga.
Akizungumza na blog ya janejohn5 jana Mkurugezi wa Kampuni ya DATK Intertaimeint, Asha Kigundula, alisema kuwa maandalizi yashindano hilo yanaendelea vizuri.
Kigundula alisema kuwa walimu watakaosimamia warembo hao ni Miss Tanga 2012 Teresia Kimolo na Mwanaid Omar.Alisema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri, ambapo
warembo wameanza kuitikia wito wa kushirikishi shindano hilo.
Kigundula alisema kuwa mpaka sasa jumla ya warembo 8 wamejitokeza kushiriki shindano hilo ambapo nafasi bado iko wazi kwa wasichana wote wenye sifa za kushiriki.
Alisema kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo mkoani humo kwa kuwa Kampuni DATK imejipanga, hivyo mashabiki wa mashindano ya urembo wa jijini hapo kwa ujumla wakae mkao wa kupata raha.
Pia alisema fomu zinapatika katika ofisi ya Mwananchi iliyopo Bandari Tanga ghorofa ya Nne, Five Brathers kwa Nassa Makau iliyopo jijini humo, kwa Dar es Salaam zinapatikana katika ofisi za Jambo Leo zilizopo Jengo la Hifadhi Hause Posta.
Shindano hilo limedhaminiwa na Redd's, CXC Africa& Tours, Tanga Beach Resorts, Lavida Pub, Jambo Leo,Staa Spoti,Cloud's Media Group, pamoja na Blog Michuzi Media Group, Bongostaz.com, Saluti5,Kajuna, JaneJohn5, na Kidevu

0 maoni:
Post a Comment