SHINDANO la mkutafuta malkia wa Mkoa wa Tanga mwaka huu
"Redd's Miss Tanga 2013" litafanyika Juni 22 kwenye Uwanja wa
Mkwakwani,Mkoani humo.
Akizungumza na gazeti hili jana Mkurugezi wa Kampuni ya DATK
Intertaimeint, Asha Kigundula, alisema kuwa warembo tayari wameanza mazoezi
yakatofanyika kwenye Ukumbi wa Lavida uliopo jijini Tanga.
Kigundula alisema shindano hilo litaanza saa 2, usiku, ikiwa
ni pamoja na kuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa moja ya bendi maarufu hapa
nchini pamoja na wasanii wanaotamba katika muziki wa kizazi kipya.
Alisema maandalizi ya shindano hilo yanaendelea vizuri jumla
ya warembo 14 watashindania taji hilo. Kigundula alisema kuwa mpaka juzi warembo 10 wamejitokeza na
kuanza mazoezi yanayosimamiwa Miss Tanga
2012 Teresia Kimolo na Mwanaid Omar.
Hawa Ramadhan (18),Hazina Mbaga (19)Like Abdulraman (19),
Jack Emannuel (18),Waida Mmbwambo(20), Tatu Hussein(19), Mwanahamis
Mashaka(20), Neema Abdallah (18), Winfrida Gutram (21)Lulu Mbonea (19) na Aisha
Rashid (21).
Redd's, Miss Tanga, imedhaminiwa na CXC Africa, Executive
Solutions,Busta General Supply, Mkwabi Interprises,Lusindic Investment LTD,
Lavida Pub, Jambo Leo,Staa Spoti,Five Brothers Cloud's Media Group, pamoja na Blog Michuzi Media Group,
Bongostaz.com, Saluti5,Kajuna, JaneJohn5, na Kidevu.
0 maoni:
Post a Comment