TAMASHA la Mastaa chipukizi la mwezi Mei litafanyika
tarehe 26,mwezi huu katika ukumbi wa Starlight Hotel kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 10 jioni.
Vikundi vya sanaa vya Kaole, Splendid, Super Shine
Taarab, Five Star Modern Taarab pamoja na wasanii mbalimbali wa Bongo Flava, Maigizo, Ngoma,
Dansi na Sarakasi wamethibitisha kushiriki tamasha hilo.
Wasanii wakongwe wa bongo flava kama Stara Thomas, Bendi
ya Msondo Ngoma na waigizaji wakongwe wa Kaole na Splendid wataonesha umahiri
wao katika fani ya sanaa.
Kauli Mbiu ni Kilio cha Msanii ambako mpaka sasa vikundi 30 kutoka jiji la Dar es Salaam vitashiriki katika tamasha hilo.
SHIWATA pia inawapongeza wote walioshiriki
tamasha la Aprili 27 ambako zaidi ya
wasanii 300 walishiriki kuonesha vipaji vyao ambako mgeni rasmi alikuwa mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM kutoka Wilaya ya Kinondoni, Calist Lyimo ambaye alitumia nafasi hiyo kuwaasa
wasanii kujituma kuonesha uwezo wao katika kuelimisha jamii.
Pia Shiwata imeupongeza uongozi wa Shirikisho la
Filamu Tanzania (TAFF) kwa ushirikiano wao mzuri na kuwaomba viongozi wengine
wa bendi za muziki, taarab,vikundi vya sanaa,mapromota,maprodusa na wadau wote
kutoa ushirikiano katika matamasha haya ili kujenga ushirikiano wa pamoja.
Maandalizi ya tamasha hilo
yamekamilika ambako wasanii kutoka vikundi mbalimbali wamepiga kambi ya kujifua
ili kuonesha ubunifu wao katika tamasha hilo.
Wakati huo huo SHIWATA inatarajia kuhamisha tamasha hilo kwa mwezi Juni kufanyikia
mkoa wa Arusha ili kuwapa nafasi wasanii wa mkoa huo nao kuonesha uwezo wao.
Wasanii
100 ambao wamefanya vizuri katika matamasha mawili yaliyokwisha fanyika
Dar es Salaam watapatiwa nafasi katika tamasha la Arusha ambalo
linafanyika 29/6/2013.
0 maoni:
Post a Comment