Sir Alex Ferguson atastaafu kama Meneja
wa Manchester United baada kudumu kwa Miaka 26 lakini atabakia Klabuni
hapo kama Mkurugenzi na Balozi Maalum.
Akitangaza kustaafu, Ferguson, Miaka 71, alisema: “Uamuzi wa kustaafu nimeufikiria sana. Wakati umefika!” Mara baada ya kutangazwa kustaafu kwake,
uvumi umeanza kuzagaa kuwa Mrithi wake ni Jose Mourinho huku wengine
wakimtaja Meneja wa Everton David Moyes na yule wa Borussia Dortmund
Jurgen Klopp.
FERGUSON-MATAJI YAKE:
-PREMIER LEAGUE: 1993, 1994, 1996, 1997, 1999,
2000, 2001, 2003, 2007, 2008, 2009, 2011, 2013.
-FA CUP: 1990, 1994, 1996, 1999, 2004
-LEAGUE CUP: 1992, 2006, 2009, 2010
-UEFA CHAMPIONS LEAGUE: 1999, 2008
-UEFA CUP WINNERS CUP: 1991
-FIFA CLUB WORLD CUP: 2008
-UEFA SUPER CUP: 1992
-FIFA INTER-CONTINENTAL CUP: 1999
-FA CHARITY/COMMUNITY SHIELD: 1990, 1993, 1994, 1996, 1997, 2003, 2007, 2008, 2010, 2011
Ferguson atastaafu rasmi kwenye Mechi
yake ya mwisho ya BPL, Barclays Premier League, hapo mei 19
watakapocheza na West Bromwich Albion wakiwa ni Mabingwa baada ya kutwaa
Ubingwa wao wa 20 katika Historia ya Klabu huku Ferguson akitwaa Mataji
13 kati ya hayo na kuifanya Man United iongoze kwa Mataji mengi.
FERGUSON KATIKA NAMBA:
1: Kutunukiwa Cho cha SIR na Malkia Jun1 1999
2: Kushinda UEFAChampions League dhidi ya Bayern Munich Mwaka1999 na Chelsea Mwaka 2008
4: League Cups
5: Timu alizokuwa Meneja: East Stirling 1974, St Mirren 1975-78, Aberdeen 1978-1986, Scotland 1985-86, Man Utd 1986-2013
6: Klabu alizocheza Kama Mchezaji - Queens Park, St Johnstone, Dunfermline, Rangers, Falkirk, Ayr.
17: Gemu alizokosa kama Meneja kwa Vifungo
26: Miaka iliyopita hadi Ferguson anaiwezesha Man United kutwaa Ubingwa 1993
27: Miaka aliyodumu Old Trafford
38: Vikombe alivyoshinda Old Trafford.
49: Vikombe alivyoshinda kama Meneja wa ManchesterUnited, Aberdeen na St Mirren.
104: Wachezaji
aliowanunua akiwa Manchester United- wa kwanza ni Liam O'Brien, kwa
Pauni £60,000 kutoka Shamrock Rovers hapo Novemba 1986 na wa mwisho ni
Wilfried Zaha toka Crystal Palace kwa Pauni Milioni 15.
170: Magoli aliyofunga kama Mchezaji
370: Mechi alizocheza kama Mchezaji.
1498: Mechi alizosimamia kama Meneja Manchester United: Ushindi 894, Sare 337 na Kufungwa 267






0 maoni:
Post a Comment