Friday, May 31, 2013

TFF YAIOMBA COREFA KUFUTA KESI MAHAKAMANI COREFA YASEMA HAWAHUSIKI NA KESI ILIVYOKO MAHAKAMANI

Baada ya shirikisho la soka hapa nchini kuamriwa na mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Pwani kusimamisha ligi ya mabingwa ya mikoa Tff imekiandikia chama cha soka mkoa wa pwani waambia wadau wa soka waliofungua kesi mahakani kufuta kisi hiyo kwa lengo la kutoharibu soka hapa nchini.

Kaimu katibu mkuu wa TFF Sunday Kayuni amesema wadau wa soka wanaofungua kesi mahakamani wanatakiwa kufahamu sheria za soka zinataka nini na hasara ya kufungua kesi mahakamani inayohusiana na soka.

Kufuati akauri ya TFF kuwata COREFA kufuta kesi mahakamani COREFA wamesema wao hawawezi kuwaambia wadau hao kufuta kesi mahakamani kwa timu ya Kiluvya iliyoondolewa katika mashindano hayo siyo mwanachama wa COREFA bali uwanachama wao uko wilayani.

Kufuatia barua kutoka TFF COREFA imekiandikia barua chama cha soka cha wilaya KIBAFA kuwaambia wadau hao kufuta kesi hahakamani.

Wadau hao walifungua kesi mahakamani kupinga ligi ya mabingwa wa mikoa kufuatia mkoa wa Pwani kupeleka timu ya Kiluvya ambayo hakukidhi vigezo vya kushiriki ligi hiyo na TFF inaaamua kuiondoa timu ya hiyo katika mashindano baada ya kupelekewa malalamiko

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU