Wazee wa klabu ya yanga imetoa tamko juu ya mchezo wa marudiano wa watani wa jadi ambapo wazee hao walianza kutoa pongezi kwa Viongozi wa Klabu
ya YANGA chini ya Mwenyekiti Yusuf Manji na Makamu Mwenyekiti Clement Sanga kwa
kuongoza Klabu na kuweza kunyakua Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu wa
mwaka 2012/2013.
Akizungumza kwa niamba ya wazee wenzake Ibrahim Akilimali amesema ubingwa wa yanga umetokana na Uongozi bora, uwajibikaji katika
kutekeleza majukumu ya Klabu na kufikia malengo.
Mwenyekiti wetu ametujengea dhana ya kuwa na imani ndani
ya Uongozi, wanachama na wachezaji wetu.Hivyo basi na sisi kama wazee wa Klabu tunayo imani na
viongozi na wachezaji wetu na tunaahidi kuwa mchezo wetu wa tarehe 18 Mei 2013
kati yetu na Simba lazima tushinde ili tusherehekee Ubingwa wetu kwa furaha,
shangwe na nderemo.
Sherehe haitakuwepo kama watashindwa kumfunga myama mei 18 uwanja wa taifa
“YANGA
DAIMA MBELE NYUMA MWIKO”






0 maoni:
Post a Comment