Mabingwa wa Bonanza la Castle Lager
Soka Fest,Fastjet wakishangilia na Kikombe mara baada ya kuibuka mabingwa
katika Bonanza hilo lililofanyika katika Viwanja vya Posta Kijitonyama Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki.
TIMU ya soka ya Shirika la Usafirishaji wa Anga Fastjet
imetwaa ubingwa wa Castle Lager Soka Fest Bonanza 2013 lililofanyika jana
Jumamosi kwenye viwanja vya Chuo cha Posta jijini Dar es Salaam baada ya
kuifunga timu ya Infinity Communications mabao 2-1 katika mechi ya fainali.
Infinity Communications walianza kupata bao la kwanza
kupitia kwa Rahim Shaaban huku Fastjet wakisawazisha kupitia kwa Kelvin Kessy.
Fastjet walipata bao la pili na kutwa ubingwa wa
bonanza hilo lililofungwa na Ally Ruvu.
Kwa kutwaa ubingwa huo, Fastjet walikabidhiwa Kombe,
medali za dhahabu, wakati mshindi wa pili Infinity Communications walipata
medali ya fedha na wa mshindi wa tatu BMF waliapata medali za shaba.
Nafasi ya tatu katika bonanza hilo ilichukuliwa na BMF
walioifunga Alpha kwa penalti 3-1, baada
ya kutoka sare ya mabao 2-2.
Awali bonanza hilo lilifunguliwa na Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Ridhiwani Kikwete, ambaye alikuwa
mgeni rasmi.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa bonanza hilo, Ridhiwani alisema michezo ni afya na
kuwataka wanamichezo hao kushiriki michezo mara kwa mara.
“Michezo inajenga afya zetu, mimi binafsi huwa nashiriki
michezo, jambo hili ni zuri, nawatakia kila la kheri katika ushiriki wa bonanza
hili,” alisema.
Kwa upande wake, Meneja wa Castle Lager, Kabula
Nshimo, alisema bonanza hilo hufanyika kila mwaka na kwa mwaka huu lilianzia
katika mikoa ya Mwanza, Iringa na kumalizikia Dar es Salaam.
“Mwaka huu bonanza hili limeshirikisha makampuni 16 na
tunatarajia mwakani makampuni mengi zaidi yatashiriki kwani mwamko umekuwa
mkubwa na tunawahimiza waendelee kuinga mkono kwa kuendelea kunywa Castle
Lager,” alisema alisema.
Timu zilizoshiriki katika bonanza hilo ni Taswa FC,
Fastjet, Infinity Communications, DSTV, TBL, NSSF, Police Dar, IPP, BMF, KCB
Bank, Gelod, Coca Cola, Aim Group, Facebook, Stanbic bank na Alpha.
Bonanza hilo lilipambwa na burudani kutoka Kalunde
band na African Stars band ‘Twanga Pepeta’.
0 maoni:
Post a Comment