Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akipokea Salamu za heshima kutoka kwa wahitimu wa mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi namba 20 katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyo fanyika katika chuo cha Magereza Kiwira Tukuyu Rungwe Mkoani Mbeya
Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akikagua wahitimu wa mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi
namba 20 katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyo fanyika katika
chuo cha Magereza Kiwira Tukuyu Rungwe Mkoani Mbeya
Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akimtunuku cheo cha Ukoplo Askari B4448 Patric Babara kwa niaba ya wahitimu wa mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi
namba 20 katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyo fanyika katika
chuo cha Magereza Kiwira Tukuyu Rungwe Mkoani Mbeya
Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akimtunuku cheti muhitimu B7348 Patrick Chalemta aliye fanya vizuri masomo ya Darasani katika mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi
namba 20
Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akimtunuku cheti
muhitimu aliye fanya vizuri somo la kulenga shabaha 3163 Tatu Amri katika mafunzo ya
uongozi daraja la kwanza kozi
namba 20
Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akimpa zawadi
muhitimu 3914 Leonida Hillu ya mwnafunzi mwenye Nidhamu usafi na ukakamavu katika mafunzo ya
uongozi daraja la kwanza kozi
namba 20
Baadhi ya Maofisa wakitoa heshima katika mahafali ya mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi
namba 20 katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyo fanyika katika
chuo cha Magereza Kiwira Tukuyu Rungwe Mkoani Mbeya
Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga (kushoto) akiwa na Mkuu wa Chuo cha Magereza Kiwira Staniford Ntirudura wakipokea Salamu za
heshima kutoka kwa wahitimu wa mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi
namba 20 katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyo fanyika katika
chuo cha Magereza Kiwira Tukuyu Rungwe Mkoani Mbeya
Wahitimu wakiwa kwenye Gwaride wakipita kwa mwendo wa Haraka mbele ya Mgeni Rasmi.
"Hima..... Hima.... Hima!.... " Ni salamu ya utii ikiongozwa na Parade Kamanda SP Lucas Ndoteela
Baadhi ya Maofisa wakifuatilia kwa Makini shughuli za Mahafali
Baadhi ya Wahitimu wakionesha umahili wa kupambana na maadui
Watoto wanaolelewa na kituo cha malezi ya watoto wadogo katika chuo cha Magereza wakitumbuiza katika Sherehe za Mahafali
Mkuu wa Chuo cha Magereza Kiwira, Kamishina msaidizi wa Magereza Staniford Ntirudura akizungumza jambo katika mahafali hayo.
Wahitimu wa mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi namba 20 katika
sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyo fanyika katika chuo cha Magereza
Kiwira Tukuyu Rungwe Mkoani Mbeya, wakifuatilia matukio yanayo endelea katika Sherehe zao.
Wahitimu B5414 Peter Ndalahwa na 3469 Matha Mwanjala wakisoma Lisara katika mahafali yao
Muhitimu B3494 Willy Timoth akisoma Shairi wakati wa mahafali
Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akizungumza na wahitimu
********************
JUMLA ya Askari 984 wa Jeshi la
Magereza, wanaume 845 na wanawake 139
wametunukiwa Vyeo vya Ukoplo
baada ya kuhitimu mafunzo ya Uongozi daraja la Kwanza kozi namba 20 katika Chuo
cha Magereza Kiwira Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya.
Vyeo hivyo vilitolewa na
Kamishina wa Fedha na Utawala Gaston Sanga kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa
Magereza katika Sherehe za ufungaji wa mafunzo hayo zilizofanyika katika
Viwanja vya Chuo hicho leo Juni 7, Mwaka huu.
Akizungumza katika mahafali
hayo, Kamishina wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga amesema Askari wa
Jeshi la Magereza Nchini wanatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili,
taratibu na kanuni za kazi kwa kufuata uwajibikaji, unyenyekevu, ukakamavu,
ujasili, upendo, ushirikiano, uvumilivu, uaminifu na nidhamu.
Kamishina Sanga amesema
Maaskari wanapaswa kuzingatia elimu waliyopewa wakati wa mafunzo ili wakawe
mfano kipindi cha utendaji kazi wao ikiwa ni pamoja na kuhamasisha na
kuwaongoza wenzao ambao hawakupatiwa elimu kama yao.
Aidha amewaasa kutowatesa
Wafungwa walioko magerezani bali kuwahudumia kwa kuzingatia kuwa wanamhudumia
binadamu kama walivyo wao na siyo
kuchukua nafasi ya kuwanyanyasa bila kuogopa haki na Stahili za binadamu
japokuwa ni wafungwa.
0 maoni:
Post a Comment