Saturday, June 8, 2013

HOYCE TEMU AKONGA NYOYO ZA WASHIRIKI WA SEMINA YA ‘How To Find Your Destiny’.

IMG_0103
Mwendesaji wa semina ya “How To Find Your Destiny” Hoyce Temu akisikiliza utambulisho kutoka kwa washiriki waliohudhuria semina hiyo ambao baadhi yao ni wajasiriamali, waajiriwa wa serikali, Mentors na wanafunzi wa vyuo. Semina hiyo imefanyika kwenye Taasisi ya Mara Foundation ya jijini Dar.
IMG_0131
Pichani juu na chini ni Mwendeshaji wa semina ya “How To Find Your Destiny” Hoyce Temu aki-share experience ya maisha yake mpaka hapo alipofika baada ya kupitia vikwazo vingi, kuvuka mabonde na malima wakati wa semina hiyo.
IMG_0133
IMG_0121
Pichani juu na chini ni Washiriki wa semina ya “How To Find Your Destiny” wakifuatilia kwa umakini shuhuda na mifano mbalimbali ya maisha iliyokuwa ikitolewa na Mwendeshaji wa Semina hiyo Hoyce Temu(hayupo pichani).
IMG_0130
IMG_0171
Mwendeshaji wa Semina ya “How To Find Your Destiny” Hoyce Temu akigawa kitabu chake kinachoelezea historia ya maisha yake kinachoitwa "Nayakumbuka Yote" ambacho kinauzwa katika maduka mbalimbali ya vitabu jijini Dar na Pesa inayopatikana katika mauzo hayo asilimia 80 inakwenda kulipia ada za shule kwa wasichana ambao ni mayatima na asilimia 20 inakwenda kwa mchapishaji.
IMG_0175
Mmoja wa washiriki akimpongeza Hoyce Temu kwa ujasiri aliokuwa nao na mateso aliyopitia katika maisha yake mpaka kufikia hapo alipo.
IMG_0184
Hoyce Temu akisaini autograph kwa mmoja washiriki.
IMG_0195
Hoyce Temu akishow love na Mmiliki wa Beutylicious Saloon iliyopo Mikocheni B Irene Juliet Mbuya.
IMG_0194
Pichani juu na chini ni Baadhi ya washiriki wakipata picha ya ukumbusho na Mrembo wa zamani aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania mwaka 1999 Hoyce Temu.
IMG_0188
Vijana jijini Dar es Salaam wamepata fursa ya kushiriki katika semina iliyoandaliwa na Mikono Business Consult kwa ajili ya kuwapa hamasa na kuwataka wasikate tamaa ili wajipange na kuangalia nini wanachotaka kukifanya katika maisha yao.
Semina hiyo iliyoendeshwa na Miss Tanzania wa zamani na Communication Analyst wa Umoja wa Mataifa Tanzania Bi. Hoyce Temu ilifahamika kwa jina la “How To Find Your Destiny” imeonekana kuwavutia washiriki waliohudhuria kutoka sehemu mbalimbali.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU