Picha ya pamoja kati viongozi wa makampuni ya ‘Nexus
Consulting Agency’ na ‘Rockstar 4000′ na wasanii wa kundi la Orijino
Komedi mara baada ya kutolewa kwa taarifa ya kundi hilo kuingia mkataba
na makampuni hayo.
Mkuu wa Kitengo cha Vipaji na Uendelezaji wa Biashara wa
Kampuni ya Rockstar 4000 Bi. Christine Mosha “Seven” akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo ambapo amesema
amefurahishwa sana kufanya kazi na Orijino Komedi ambao ni watu wenye
vipaji vya hali ya juu na kuingia mkataba na Kampuni ya Nexus Consulting
Agency ambapo kwa pamoja wamedhamiria kukuza na kubadilisha dhama ya
vipaji na sanaa kutoka ilipo na kuwa ya kimataifa. Kushoto ni Mkurugenzi
Mkuu wa Nexus Agency Bw. Bobby Bharwani na kulia ni Muandaaji wa
vipindi vya Orijino Komedi Sekioni David.
Mkurugenzi Mkuu wa Nexus Consulting Agency Bw. Bobby
Bharwani (kushoto) akieleza kuwa kwa upande wa kampuni yao kushirikiana
na Orijino Komedi ni kitu muhimu kwa Nexus kwani siku zote imekuwa
ikitamani kufanya kazi kwa karibu na kundi hilo na kuthamini kazi zao
kutokana na vipaji vya hali ya juu walivyokuwa wakionyesha wasanii wa
kundi hilo.
Kundi la kipaji cha Televisioni
“Orijino Komedi” linaloongoza nchini kwa vipindi vyake kupitia
televisionilimeingia mkataba na Kampuni ya Nexus Consulting Agency kwa
kushirikiana na Rockstar 4000, ambao utakuwa ni mkataba wa kwanza kwa
wasanii wa luninga kupitia kampuni ya Nexus.
Nexus imenunua haki zote za
usimamizi wa biashara na uongozi wa kundi hilo ambalo linajulikana sana
nchini kupitia vichekesho vyake vinavyoonyeshwa na vituo vya television
na matamasha mbalimbali, ambapo mkataba huo utakuwa ni kwa ajili ya
kusimamia kipindi hicho cha vichekesho kinachoundwa na wachekeshaji saba
ambao ni Joti, Macreagan, Masanja, Wakuvanga, Mpoki, Vengu na Seki
David ambacho kimekuwa hewani kwa mfululizo wa miaka sita.
Kwa kushirikiana na Rockstar 4000,
Nexus imesema itahakikisha inaendeleza vipaji vya wasanii wa kundi hilo
ili vipaji vyao viweze kufikia kiwango cha juu cha ufanisi ndani ya
Afrika na Kimataifa kwa ujumla.
0 maoni:
Post a Comment