Mwenyekiti
wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete,
akiongoza kikao cha Maalum ya CCM 'Kamati Kuu' kilichokutana jana usiku
mjini Dodoma kwa ajili ya kuipokea Rasimu ya Katiba mpya,
iliyosomwa hivi karibuni. Picha na www.sufianimafoto.com
Kamati
Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imekutana jana tarehe 10/06/2013
chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dr. Jakaya Mrisho
Kikwete. Kikao hicho kilikuwa cha siku moja na maalum kwa ajili ya
kupokea rasimu
ya katiba mpya.
Kamati
Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imekutana jana tarehe 10/06/2013
chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dr. Jakaya Mrisho
Kikwete. Kikao hicho kilikuwa cha siku moja na maalum kwa ajili ya
kupokea rasimu ya katiba mpya.
Kamati Kuu inaipongeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini kwa kazi nzuri na kukamilisha kazi kwa wakati.
Kamati Kuu imepokea rasimu hiyo na kuelekeza kuwa; Kwa kuwa rasimu hii ni ya kwanza ambayo inapelekwa kujadiliwa tena
kwa wananchi kupitia mabaraza mbalimbali ya katiba baada ya kuisha kwa hatua ya kutoa maoni.
Kamati
Kuu imekiagiza Chama kijipange kuijadili rasimu hiyo ndani ya Chama
kama baraza la kitaasisi la katiba na kuwataka wanachama na wapenzi wa
CCM wajitokeze kwa wingi na kushiriki kwenye mabaraza haya.
Ushiriki huu wa
CCM baada ya kupokea rasimu umekusudia kushirikisha wanachama wetu kwenye ngazi ya tawi, wilaya, mkoa na Taifa.
Lakini
pia Jumuiya za CCM zimekusudia kushiriki kama mabaraza ya Katiba na
hivyo kuongeza ushiriki wa wanachama na wapenzi wa CCM katika mchakato
huu.
CCM kama baraza la katiba la kitaasisi litaipitia rasimu iliyowasilishwa kifungu kwa kifungu
na kwa kuzingatia maoni ya CCM
yaliyotolewa mwanzoni kabisa mwa mchakato wa mabadiliko ya Katiba,
wanachama wetu watashiriki kutoa maoni yao.
Pamoja
na kazi nzuri ya Tume ya Mabadiliko ya katiba, Kamati Kuu inaiomba Tume
hiyo kueleza vizuri mchakato mzima kutoka rasimu ya kwanza mpaka rasimu
ya mwisho ili kuondoa mkanganyiko kwa wananchi juu ya mchakato mzima
hasa baada ya rasimu ya kwanza kutoka.
Kamati
Kuu inawasihi Watanzania kushiriki tena kwenye kutoa maoni kupitia
mabaraza ya katiba kwa rasimu ya kwanza, bunge maalum la katiba kwa
rasimu ya pili na kupitia kura ya maoni kwa rasimu ya tatu, kwa
amani,utulivu na kuvumiliana ili mwisho wa siku tupate Katiba nzuri ya
nchi yetu kwa masilahi ya Watanzania walio wengi.
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Moses Nnauye, akizungumza na waandishi
wa habari mjini Dodoma leo mchana kuhusu kikao hicho cha Kamati Kuu ya
CCM, kilichokutana jana usiku.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu, waliohudhuria kikao hicho jana usiku.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, Mwigulu Nchemba,
akiperuzi 'mambo flani' katika simu yake ya mkononi, wakati akiwa
ukumbini humo kwenye Kikao cha Kamati Kuu kilichokutana jana usiku.
Sehemu ya Wajumbe wa Kikao hicho ambao wengi wao ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
0 maoni:
Post a Comment