Warembo
wa Redds Miss Kinondoni 2013 wakitambulishwa kwa Naibu Mustahiki Meya
wa Manispaa ya Kinondoni Mheshimiwa Songolo ambaye alimwakilisha mgeni
rasmi meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda. Mgeni huyo pia
alipata fulsa ya kuzinduliwa rasmi kambi ya Redds Miss Kinondoni 2013
iliyopo katika hoteli ya JB Belmont jijini Dar es Salaam.
Naibu
Mustahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mheshimiwa Songolo ambaye
alimwakilisha mgeni rasmi meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda
akiongoza harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kununua vitanda kwa
ajili ya akina mama wanaojifungua (delivery beds) kwa hospitali za
Mwananyamala pamoja na Sinza Palestina ambapo warembo hao walitembelea
wodi za akina mama na kufanya usafi. Pamoja na harambee kulizinduliwa
rasmi kambi ya Redds Miss Kinondoni 2013. Pembeni ni Mkuu wa Itifaki wa
Mashindano ya Miss Tanzania, Albert Makoye na Mratibu wa shindano
la Redd's Miss Kinondoni Bw. Ssebo. Harambee hiyo ilifanyika ukumbi wa
Ambassador uliopo hoteli ya JB Belmont jijini Dar es Salaam.
Jumla
ya vitanda 15 vyenye thamani ya shilingi milioni 52.5 zimepatikana
katika harambee iliyoandaliwa na warembo wa Redds Miss Kinondoni 2013
kwa ajili ya kununua vitanda kwa ajili ya akina mama wanaojifungua
(delivery beds) kwa hospitali za Mwananyamala pamoja na Sinza Palestina
iliyofanyika katika ukumbi wa Ambassador uliopo hoteli ya JB Belmont
jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
mshiriki wa shindano hilo, Sarah Paul alisema kuwa wanamshukuru Mungu
kwa kuweza kuwawezesha kufanya harambee hiyo ambayo ilitokana na wao
baada ya kutembelea hospitali ya Mwananyamala pamoja na Sinza Palestina
wakajionea uhaba wa vitanda vya akina mama wakati wa kujifungua.
"Tulisononeshwa
sana na hali tuliyoikuta hospitalini hapo ambapo baada ya kuongea na
mganga mkuu wa Manispaa ya Kinondoni dokta Gunini Kamba alitueleza kuwa
jumla ya akina mama wapatao 50 mpaka 80 hujifungua kwa siku moja hivyo
wanauhaba wa vitanda, tukaona tukae na viongozi wetu watusaidie kuandaa
harambee na tunamshukuru Mungu tumefanikiwa kupata vitanda 15 japo nia
yetu ilikuwa ni kupata vitanda 20," alisema mrembo huyo.
Warembo wa Redds Miss Kinondoni 2013 walipata fulsa ya kucheza mara baada ya harambee na ufunguzi rasmi ya kambi yao.
Furaha zilitanda.
Kila mmoja akionyesha ufundi wake.
Mashindano
ya Redd's Miss Kinondoni 2013 yamedhaminiwa na Redd's Original, Chilly
Willy Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products, Times Fm, JB
Belmonte Hotel, Michuzi Media Group, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog,
Fullshangwe Blog, HandeniKwetu Blog, Mrokim Blog, TheHabari.com,
JestinaGeorge Blog, SufianMafoto Blog, Global Publisher, Mdimuz Blog,
Lukaza Blog, MO Blog na Kajunason Blog.
0 maoni:
Post a Comment