· Mawasiliano ya radio yaboreshwa kufikia vijiji vingi zaida kulinganishwa na awali
· Zaidi ya radio 8 kuzindua chini ya mradi huu
Jumanne 16
Julai 2013 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na
shirika lisilo la kiserikali UNESCO wanatarajia kuzindua radio jamii
katika wilaya ya Karagwe mkoani Bukoba mwishoni mwa wiki hii
Uzinduzi
huo unafatia ushirikiano kati ya Airtel na UNESCO katika mradi wa
kusadia jamii na kufikisha mawasiliano ya radio sehemu ambazo zina
changamoto za huduma za mawasiliano ya radio
Akiongea
kuhusu uzinduzi huo ya Airtel Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Airtel
Beatrice Singano alisema “ Mradi huu wa radio za jamii tunaufanya kwa
kushirikiana na UNESCO kwa lengo la kuendeleza na kuboresha huduma za
mawasiliano na kuwafikia wananchi wengi zaidi hususani wa maeneo ya
vijijini.
Tumejipanga
kufanya uzinduzi wa ushirikiano wetu na UNESCO na Radio ya FADECO
Karagwe utakaofanyika siku ya Ijumaa tarehe 19 julai 2013
Mgeni
rasmi atakuwa ni mkuu wa mkoa wa Bukoba LutenFabian Masawe , pamoja na
yeye tutakuwa na viongozi mbalimbali wa serikali watakaohuduria sherehe
za uzinduzi huo
Tunaamii
kwa kupitia radio hizi jamii itabadilika na kupata elimu zitakazosaidia
kuleta maendeleo katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu wananchi wengi
wana pata habari mbalimbali zikiwemo za kibiashara, uchumi, kijamii na
kisiasa.
Afisa mradi wa habari na mawasiliano UNESCO Yusuph Al Amin
alisema “tunayo miradi mingi ya kusaidia jamii kujikwamua na hali ngumu
za uchumi, kupata elimu bora, uongozi bora , kuachana na mila potofu na
mengine mengi. kwa kupitia mradi huu wa Radio tunaoshirikiana na
wenzetu wa Airtel tumeshaona matunda na mafanikio mengi mpaka sasa,
lengo letu ni kuhakikisha tunatatua changamoto zilizopo za kuwapata
wananchi habari za ndani na nje ya nchi na kuwaunganisha na sehemu
nyingine za nchi na Dunia.
Akiongea
kuhusu uzinduzi wa Radio jamii Karagwe Mkurugenzi wa Radio ya FADECO Bw
Joseph Sekiku alisema “Mpaka sasa vifaa na mitambo ya mawasiliano ya
kisasa imeshafungwa na tuko katika hatua ya majaribio ambapo
tumeshuhudia ufanisi mkubwa zaidi kulinganisha na awali kwani tumeweza
kutanua wigo na kufikia vijiji vingi zaidi”.
nawashukuru
sana Airtel na UNESCO kwa kutufikia na kuwawezesha kuendesha radio yetu
kwa ufanisi zaidi. Radio ya FADECO ilizinduliwa toka mwaka 2007 na
kuanza kurusha matangazo yetu rasmi kwa vijiji vya karibu, changamoto
tuliyokuwa nayo ni pamoja na kurusha matangazo yetu katika vijiji
vilivyo mbali zaidi kutoka hapa radioni. Kwa kupitia mradi huu tumeweaza
kuona mfanikio makubwa tayari,
“Tunagemea
kuzindua rasmi ushirikiano wetu na UNESCO pamoja na Airtel siku Ijumaa
hapa Karagwe. Nachukua fulsa kuwaalika wananchi wadau wa sekta za
mawasiliano, viongozi mbalimbali kuhudhuria halfa hii ya uzinduzi na
kusherehekea pamoja nasi mafanikio haya” aliongeza Sekiku
Mradi
wa radio jamii umeanzishwa mwaka jana 2012 radio zaidi ya 10 katika
maeneo mbalimbali ya nchi zitafaidika na mradi huu kama ilivyo katika
Radio hii ya FADECO iliyopo wilaya ya Karagwe Bukoba
0 maoni:
Post a Comment