WANAMUZIKI Nguli nchini wakiongozwa
na Sit bin Saad ambaye ni mjukuu wa
marehemu Bi.Kidude,Synerg,Baby J wote hawa ni kutoka Zanzibar Linah na THT Band kutoka Dar es Salaam kesho
watawasha moto ndani ya mabo klabu kwa ajili ya
kumuenzi marehemu Bi.Kidude ambaye aliwahi kutumbuiza katika matamasha
ya ZIFF yaliyowahi kufanyika.
Tamasha la filamu la nchi za Jahazi maarufu
kama ZIFF linaendelea kupamba moto na kesho ni usiku maalumu wa wanawake katika
kumuenzi marehemu Bi.Kidude katika
tamasha hilo.
Tamasha hilo ambalo lina siku ya 5 tangu
kuanza kwake limekuwa ni kivutio kikubwa kwa wakazi na wageni kutoka kila kona
ya dunia kuwapa burudani kulingana na
mahitaji.
Usiku
wa wanawake unatarajia kufanyika jioni ya leo ndani ya Mambo klabu
ampapo wasanii watakao tumbuiza katika tamasha hio watakuwa ni wanawake
pekee ambapo mjukuu wa marehemu Bi.KIdude atafungua dimba
kutoa burudani hiyo.
Wanawake wameombwa kuhudhuria kwa wingi
kwakuwa tamasha la siku ya leo ni kwa
ajili ya wanawake.
katika tamasha hilo la usiku wa wanawake
wasanii hao wataweza kukonga nyoyo za mashabiki wake na kufanya kufana kwa
tamasha hilo ambalo linamkumbuka Bi.kidude kwa mchango wake ambao alikuwa
akiutoa katika kipindi chake chote cha uhai wake.
Hata hivyo burudani hiyo itaambatana na
kuonyeshwa kwa filamu mbili tofauti ikiwemo ya The Last Fishing Boat kutoka
Malawi na Lilet never Happened kutoka Netherland.
0 maoni:
Post a Comment