Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limefanya mabadiliko ya mwamuzi wa mechi
ya mchujo kusaka tiketi ya Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi ya
Ndani (CHAN) kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Uganda (The Cranes)
itakayochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mwamuzi
aliyeondolewa kutokana na sababu za kiufundi ni Jean Claude Birumushahu
aliyekuwa mwamuzi msaidizi namba moja. Nafasi yake sasa inachukuliwa na
Herve Kakunze pia kutoka Burundi.
CAF
imemuondoa mwamuzi huyo baada ya kufeli katika mtihani wa waamuzi
(Cooper Test) kwa waamuzi wa Burundi wanaotambuliwa na Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) uliofanyika nchini humo siku tatu
zilizopita.
Waamuzi
hao na Kamishna wa mechi hiyo Gebreyesus Tesfaye kutoka Eritrea
wanatarajiwa kuwasili nchini kesho (Julai 11 mwaka huu) kwa ndege za
Kenya Airways na EgyptAir kwa muda tofauti.
Nayo
Uganda Cranes inatarajiwa kuwasili nchini kesho (Julai 11 mwaka huu) na
itafikia hoteli ya Sapphire. Shirikisho la Mpira wa Miguu Uganda (FUFA)
bado halijatuma taarifa rasmi juu ya ujio wa timu hiyo.
Wakati
huo huo, makocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen na wa Uganda, Milutin
Micho pamoja na manahodha wao watakuwa na mkutano na Waandishi wa Habari
utakaofanyika keshokutwa (Julai 12 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye
ofisi za TFF kuzungumzia mechi ya Jumamosi.
FRIENDS, POLISI KUCHEZA MECHI YA RCL JUMAPILI.
Mechi
ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) kati ya Friends Rangers
ya Dar es Salaam na Polisi Jamii ya Mara iliyokuwa ichezwe Jumamosi
(Julai 13 mwaka huu) imesogezwa mbele kwa siku moja.
Timu
hizo sasa zitacheza Jumapili (Julai 14 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Azam
ulioko Chamazi. Polisi Jamii ilishinda bao 1-0 mechi ya kwanza
iliyochezwa Julai 6 mwaka huu Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini
Musoma.
Refa
Hans Mabena kutoka Tanga ndiye atakayechezesha mechi akisaidiwa na E.
Mkumbukwa na Hajj Mwalukuta wote kutoka Tanga. Mwamuzi wa akiba (fourth
official) ni Kessy Ngao wa Dar es Salaam.
Mechi
kati ya Stand United FC ya Shinyanga na Kimondo SC ya Mbeya itachezwa
Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kambarage mjini
Shinyanga. Mwamuzi atakuwa Daniel Warioba kutoka Mwanza. Kimondo SC
ilishinda mechi ya kwanza bao 1-0.
0 maoni:
Post a Comment