Mkuu wa
Wilaya ya Bukoba Bi Ziporah Pangani akimkabidhi kiongozi wa kundi la
Abakambamoi Bw Projestus Boniface kitita cha shilingi laki 5 ikiwa
zawadi ya mshindi wa kwanza wa fainali
za mashindano Ngoma za Asili kwa Mkoa wa Kagera, katikati ni Afisa
utamaduni Manispaa ya Bukoba Evarisia Ruafiyami na Meneja masoko Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Ziwa Bw Andrwe Mmbwambo,Mashindano ambayo yalidhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager bia ya Kanda ya Ziwa.
Mkuu wa
Wilaya ya Bukoba Bi Ziporah Pangani akimkabidhi kiongozi wa kundi la
Ruau Bw Ezekhiah Henriko kitita cha shilingi laki 6 ikiwa zawadi ya
mshindi wa kwanza wa fainali
za mashindano Ngoma za Asili kwa Mkoa wa Kagera, katikati ni Afisa
utamaduni Manispaa ya Bukoba Evarisia Ruafiyami na Meneja masoko Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Ziwa Bw Andrwe Mmbwambo,Mashindano ambayo yalidhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager bia ya Kanda ya Ziwa.
Wasanii wakiwa kazini katika fainali
za Ngoma za Asili kwa Mkoa huo ambyo mashindano ambayo yalidhaminiwa na
kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager
bia ya Kanda ya Ziwa.
Baadhi ya Wakazi wa Manispaa ya
Bukoba Mkoani Kagera ambao walijitokeza kwa wingi katika viwanja vya
kaitaba kushuhudia fainali za Ngoma za Asili kwa Mkoa huo ambyo
mashindano ambayo yalidhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia
bia yake ya Balimi Extra Lager bia ya Kanda ya Ziwa.
Kundi la ngoma za asili
la Ruau limefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya ngoma mkoa wa Kagera chini
ya udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania
(TBL) kupitia kinywaji chake cha BALIMI EXTRA LAGER.
Kundi la Ruau limetwaa
ubingwa huo baada ya kupata alama 249 na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi.600,000/=
na tiketi ya kuwakilisha mkoa wa Kagera katika fainali za mashindano ya Kanda
yanayotarajiwa kufanyika julai 20 mwaka huu jijini Mwanza.
Washindi wa pili katika mashindano hayo ni
kundi la Abakambamoi ambao wamepata alama 227 na hivyo kujinyakulia fedha
taslimu shilingi 500,000/=nafasi ya tatu imechukuliwa na kundi la Rugomoire kwa
alama 226 na kuzawadiwa shilingi.400,000/= huku kundi la Aruta wakiondoka na
nafasi ya nne na kuzawadiwa shilingi 300,000/= .
Jumla ya vikundi 12
vimeshiriki mashindano hayo,ambapo vikundi vingine vilivyo shika nafasi ya 5
mpaka 12 vimeondoka na kifuta jasho cha fedha taslimu sh.150,000/=
Mgeni rasmi katika mashindano hayo Mkuu wa Wilaya
ya Bukoba Ziporah Pangani akizungumza na washiriki wa mashindano hayo pamoja na
wakazi wa Mkoa wa Kagara waliojitokeza kushuhudia fainali hizo ameipongeza
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager kwa
kudhamini mashindano mbalimbali na kuvitaka vikundi vilivyo shika nafasi ya
kwanza vya Ruau kutoka Karagwe na kundi lililo chukua nafasi ya pili la Abakambamoi
kutoka Muleba kwenda kuwakilisha mkoa wa Kagera vema katika mashindano hayo ya Kanda.
Ziporah amesema ni aibu
kwa mkoa huo kuwa wasindikizaji katika mashindano hayo na kuwataka maafisa
utamaduni na viongozi wa vikundi hivyo
kuhakikisha kuwa wanafanya mazoezi kuanzia sasa ili viweze kurejea na
nafasi za juu katika katika mashindano
hayo “ nawataka mreje mkiwa nafasi za juu ya kwanza mpaka ya tatu msipo pata
nafasi hizo hamto panda meri kurejea kagera”alisema Mkuu wa Wilaya huyo.
Naye Meneja masoko wa Kampuni ya Bia Tanzani (TBL) Kanda ya Ziwa Andrew Mbwambo amesema
kuwa kampuni yake imekuwa ikishiriki katika kudhamini shughuli mbalimbali
za kijamii ikiwemo michezo na burudani ikiwa ni shukrani zao kwa jamii kwa
kutumia bidhaa zao ambapo ameiomba jamii ili kampuni hiyo iweze kuendelea
kudhamini shughuli hizo wawaunge mkono kwa kutumia bidhaa zao, hasa bia ya
Balimi Extra Lager bia ya Kanda ya Ziwa pekee.
Aidha Mbwambo amewataka
wakazi wa jiji la Mwanza kujitokeza kwa wingi jumamosi hii kushuhudia mashindano
hayo ya ngoma za asili na kuwaona wawakilishi wao watakao wawakilisha katika
mashindano ya Kanda ambayo yatashirikisha mikoa 6 ya kanda ya ziwa ambapo pia
amepongeza mwitikio wa wakazi wa Kagera katika shughuli hiyo.
Vikundi vingine ambavyo
vimeshiriki katika fainali hizo ni pamoja na Rumanyika kutoka Karagwe,
Bikolwengonzi kutoka Bukoba, Tuelimishane kutoka Misenyi, Abasubi kutoka
Biharamuro, Jipemoyo Muleba, P. gaigwa, Abaligambo kutoka Bukoba na Obumoi
ngonzi .
0 maoni:
Post a Comment