Mchujo
wa kuwapata vijana wa Copa Coca Cola U-15 Mjini Moshi unatarajiwa kuanza siku
ya Jumapili ya Julai 7,mwaka huu kwa
kuzialika timu 10 kutoka mjini humo kuwania nafasi ya kupata wachezaji vipaji
kwa mchezo wa soka.
Akizungumza katika kikao cha
upangaji wa ratiba ya mchakato huo na
viongozi wa vilabu husika Mratibu wa Copa Coca Cola wilaya ya Moshi Waziri
Rashid amesema timu 10 zimethibitisha kushiriki mchujo huo.
Rashid ameongeza kuwa timu hizo
zinatarajiwa kutoa vijana chipukizi vipaji katika soka chini ya umri wa miaka
15 ambapo Julai 7 na Julai 13 mwaka huu mchujo huo utafanyika.
Mwenyekiti huyo ameongeza
kusema Uwanja wa King George Memorial ulioko Soweto
mjini Moshi mkoani humo
utatumika kutokana na uwezo wake wa kuchukua watu wengi na viwanja viwili
ambavyo vitatumika vyote kwa wakati mmoja.
Wazir amezitaja timu
zitakazoshiriki na ratiba yake kupangwa kuwa ni New Generation, Moshi Chrisc,
Kitayosce FC , Golden Kids, Deeper Life, Hard Life, Afro Kids, Amani Centre,
Reed Scorpion na UMISETA combine zote za mjini Moshi.
Hata hivyo makocha na viongozi
wa timu hizo wametakiwa wawazi katika miaka ya watoto hao ili kupata vipaji
hasa vya Copa Coca Cola U-15 kutokana na ukweli kwamba
0 maoni:
Post a Comment