Thursday, July 4, 2013

MEYA WA MANISPAA YA ILALA ATEMBELEA MAONYESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA - SABASABA

IMG_8364
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiwasili katika viwanja vya maonyesho ya 37 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea jijini Dar ambapo alitembelea mabanda mbalimbali.(Picha na Zainul Mzige).
IMG_8735
Mkurugenzi Mtendaji wa Home Shopping Centre (HSC) Fahad Said Mohamed (kushoto) akimkaribisha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa kwenye Banda la HSC kwenye maonyesho ya 37 kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
IMG_8738
Mstahiki Meya Jerry Silaa akiangalia baadhi ya bidhaa zenye ubora zinazouzwa na Kampuni ya HSC katika maonyesho ya 37 ya Kimataifa ya Biashara katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Home Shopping Centre (HSC) Fahad Said Mohamed.
IMG_8748
Mstahiki Meya Jerry Silaa akingalia kifaa cha kusafishia mazulia jinsi kinavyofanya kazi. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Home Shopping Centre (HSC) Fahad Said Mohamed.
IMG_8743
Mstahiki Meya Jerry Silaa akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Home Shopping Centre (HSC) Fahad Said Mohamed na baadhi ya wafanyakazi wa HSC katika Banda lao lililopo kwenye viwanja vya Sabasaba.
IMG_8744
Umati wa wakazi wa jijini Dar es Salaam ukiwa umefurika kwenye Banda la Home Shopping Centre kujipatia mahitaji mbalimbali ya nyumbani.
IMG_8808
Mtsahiki Meya Jerry Silaa akipewa maelezo ya jinsi Mfuko wa Fursa sawa kwa wote unavyopambana na kutokomeza Ugonjwa wa Saratani ya Matiti kwa wakina mama nchini. Kushoto ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Mama Anna Mkapa.
IMG_8797
Mstahiki Meya Jerry Silaa akisalimiana Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal walipokutana kwenye Banda la Mfuko wa Fursa sawa kwa wote (EOTF) kwenye viwanja vya maonyesho ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar.
IMG_8830
Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Mama Anna Mkapa akiagana na Mstahiki Meya Jerry Silaa mara baada ya kutembelea Banda la (EOTF) linalotoa fursa kwa wajasiriamali nchini Tanzania kuonyesha bidhaa zao katika maonyesho hayo kila mwaka.
IMG_8558
Mstahiki Meya Jerry Silaa akipata maelezo jinsi ya kutumia Kizimamoto Fanisi cha kurusha (Fire Extinguisher) ambacho ni rahisi kutumia na hakihitaji matengenezo na hudumu kwa miaka mitano pia Kifaa hicho ni rafiki wa mazingira na mvumbuzi bora kwa uokoaji wa dharura wakati alipotembelea Banda la GreenBat Fire Solutions katika maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea.
IMG_8574
Mstahiki Meya Jerry Silaa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa GreenBat Fire Solutions.
IMG_8542
Mstahiki Meya Jerry Silaa akisaini kitabu cha wageni katika banda la Arusha International Conference Centre (AICC) wanaoshughulika kutoa huduma za kumbi za Kimataifa za mikutano na Utalii jijini Arusha.
IMG_8531
Mstahiki Meya Jerry Silaa akingalia jinsi mtoto Range Jackson ( wa pili kushoto) mwenye ulemavu wa Ubongo akionyesha ramani ya Tanzania na Sehemu ya mipaka yake iliyotumika kumfundishia kujua kusoma na kuandika na ufundi stadi kupitia kituo cha VETA. Kulia ni Mkufunzi wa kuchomea (Welding Instructor) na Mwalimu wa watu wenye mahitaji maalum Bw. Kintu Kilanga na Wa tatu kulia ni Baba mzazi wa kijana huyo Bw.Jackson Range.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU