Bondia
Thomas Mashali akionesha midoli yake anayoifananisha na mabondia
wenzake, Kalama Nyilawila (kushoto) na Mada Maugo, wakati wa mazoezi
yake yanayoendelea katika gym yake iliyopo Manzese, Dar es Salaam.
BONDIA Thomas Mashali amewafananisha mabondia
wenzake, Mada Maugo na Kalama Nyilawila kama midoli kwa kuwakebehi kuwa
hawana lolote.
Hatua hiyo ya Mashali inatokana na awali kupondwa
na Maugo kuwa hana uwezo na ni heri akageukia biashara ya kuuza chapati,
wakati Kalama akimkebehi kuwa ni kibonde wake.
Akizungumza na
mwandishi wa gazeti hili katika gym yake, Manzese, Dar es Salaam jana,
Mashali alisema mabondia hao hawana uwezo wa kupambana naye kwa sasa na
ni kama midoli kwake.
Mashali, ambaye atapanda ulingoni Oktoba 30
katika Ukumbi wa Diamond Jubilee kuzichapa na Maugo, yuko katika
mazoezi makali kwa ajili ya pambano hilo kabla ya baadaye kupigana na
Nyilawila.
"Unajua hawa ni kama midoli kwangu (huku akionesha midoli aliyoshika), na kwa
kudhihirisha hilo nitaanza na maugo Oktoba 30 kumuonesha kuwa hatakiwi kuzungumza asichokijua," alisema Mashali.
Alisema anaamini uwezo wake wa sasa utakuwa wa juu zaidi ya Maugo na Nyilawila, ambapo alipata sare alipopigana na Nyilawila.
Katika
pambano hilo la Mashali na Maugo la Oktoba 30, kutakuwa na mapambano
mengine ya utangulizi, ambapo Ibrahim Class 'King Class Mawe' atapanda
ulingoni kupambana na Halid Manje katika mchezo wa raundi sita.
Siku hiyo kutakuwa na uhuzwaji wa DVD
mpya kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa masumbwi zitakazokuwa zikisabazwa
na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila
'Super D'
DVD hizo mpya ni kati ya
mike tyson vs evander holyfield na felix trinidad vs roy jones jr
ambapo dvd hizo zilizo rekodiwa kwa ubora wa hali ya juu kwa ajili ya kutoa mafunzo ya mchezo wa masumbwi nchin
Bondia
Thomas Mashali akionesha midoli yake anayoifananisha na mabondia
wenzake, Kalama Nyilawila (kushoto) na Mada Maugo, wakati wa mazoezi
yake yanayoendelea katika gym yake iliyopo Manzese, Dar es Salaam.
|
Bondia
Thomas Mashali akionesha midoli yake anayoifananisha na mabondia
wenzake, Kalama Nyilawila (kushoto) na Mada Maugo, wakati wa mazoezi
yake yanayoendelea katika gym yake iliyopo Manzese, Dar es Salaam. |
|
Bondia
Thomas Mashali akiwa amekumbatia midoli yake anayoifananisha na mabondia
wenzake, Kalama Nyilawila (kushoto) na Mada Maugo, wakati wa mazoezi
yake yanayoendelea katika gym yake iliyopo Manzese, Dar es Salaam picha na BLOG YA
SUPER D |
0 maoni:
Post a Comment