Wafanyakazi wa Benki ya NBC kitengo cha operesheni,
wakipozi kwa picha na watoto wanaolelewa katika kituo cha Ijango Zaidia
Orphanage cha Sinza walipokwenda kupeleka msaada wa vyakula, sabuni, mafuta ya
kupikia na vyandarua ikiwa ni moja ya mikakati ya NBC kurudisha sehemu ya faida
waipatayo katika jamii. Hafla ilifanyika kituoni hapo jijini Dar es Salaam
juzi. Wengine ni watumishi wa kituo hicho.
Mkurugenzi wa Uendeshaji na Huduma wa Benki ya NBC
Tanzania, Cornie Loots (kulia) akikabidhi msaada wa vyakula, mafuta ya kupikia,
sabuni na vyandarua kwa Mkuu wa kituo cha watoto yatima cha Ijango Zaidia
Orphanage , Bi. Zaidia Nuru Hasani, vilivyotolewa na NBC kituoni hapo, Sinza,
Dar es Salaam juzi
Mtoto anayelelewa katika kituo cha watoto yatima cha
Ijango Zaidia Orphanage, Ramia Mahmoud , akipokea mafuta ya ngozi kwa niaba ya
wenzake vyaliyotolewa msaada na Benki ya NBC kutoka kwa mfanyakazi wa benki
hiyo, Ernest Paulo Mbepera (kulia) kituoni hapo, Sinza, jijini Dar es Salaam.
Benki hiyo pia ilikabidhi msaada wa vyakula, mafuta ya kupikia, sabuni na
vyandarua.
Mfanyakazi wa Benki ya NBC, Mwanaisha Nassoro Ayosi
(kulia) akikakabidhi misaada iliyotolewa na benki hiyo kwa baadhi ya watoto
wanaolelewa katika kituo cha watoto yatima cha Ijango Zaidia Orphanage, kituoni
hapo, Sinza, Dar es Salaam juzi.
Mtoto anayelelewa katika kituo cha watoto yatima cha
Ijango Zaidia Orphanage, Amina Twahilu, akipokea moja ya vyandarua kwa niaba ya
wenzake vilivyotolewa msaada na Benki ya NBC kutoka kwa mfanyakazi wa benki hiyo,
Anyelwisye Enock Mwakatobe (kulia) kituoni hapo, Sinza, Dar es Salaam juzi. Benki
hiyo pia ilikabidhi msaada wa vyakula, mafuta ya kupikia na sabuni.
0 maoni:
Post a Comment