Wednesday, July 17, 2013

YUNA NA UNESCO YAKUSANYA MAONI YA WANANCHI WA KARAGWE KUHUSU UTEKELEZAJI WA MRADI WA AMANI NA DEMOKRASIA KWA KUSHIRIKIANA NA REDIO ZA KIJAMII (FADECO).

IMG_0073
Mshauri wa Radio Jamii kutoka UNESCO Rose Haji Mwalimu akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Dary Lwegasira alipomtembelea ofisini kwake mjini Kayanga mkoani Kagera kutambulisha mradi wa Amani na Demokrasia wenye lengo la kuhamasisha ushiriki wa jamii miongoni mwa vijana, wanawake na walemavu katika maendeleo na kudumisha amani nchini Tanzania. Mradi huo utakuwa unaratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na UNDP.
IMG_0085
Mweka hazina wa Shirikisho la Vijana la Umoja wa Mataifa (YUNA) Tanzania Bara na Visiwani Bw. Omary Hassan akifafanua jambo kuhusiana na mradi wa Amani kwa Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Dary Lwegasira (wa tatu kulia) namna utakavyoendeshwa kwa wakazi wa Wilaya yake. Kushoto ni Mkurugenzi wa Radio jamii FADECO ya Wilaya ya Karagwe Joseph Sekiku na wa pili kulia ni Mshauri wa Radio Jamii kutoka UNESCO Rose Haji Mwalimu.
IMG_0221
Picha juu na chini ni Bw. Omary Hassan akikusanya maoni ya vijana wa Chuo cha Ufundi Stadi (KDVTC) kilichopo kitongoji cha Kayanza wilayani Karagwe mkoa wa Kagera.
IMG_0182 IMG_0208
Mweka hazina wa Shirikisho la Vijana la Umoja wa Mataifa (YUNA) Tanzania Bara na Visiwani Bw. Omary Hassan na Mkurugenzi wa Radio jamii FADECO ya Wilaya ya Karagwe Joseph Sekiku (fulana ya Blue) kwenye picha ya pamoja na walimu na wanafunzi wa Chuo cha ufundi stadi (KDVTC) mara baada ya kumaliza zoezi la ukusanyaji maoni kwa wananchi wa Karagwe.
IMG_0254
Mweka hazina wa Shirikisho la Vijana la Umoja wa Mataifa (YUNA) Tanzania Bara na Visiwani Omary Hassan akizungumza na uongozi wa Perfect Education of Tourism and Institutions (PETI) kuhusiana na ukusanyaji maoni ya Utekelezaji wa Mradi wa Amani na Demokrasia Wilayani Karagwe. Kushoto ni Mkuu wa taasisi ya PETI Devotha Brassio na Makamu Mkuu wa taasisi hiyo Fravian Gedion.
IMG_0271
Bw. Omary Hassan akizungumza na wanafunzi wa Perfect Education of Tourism and Institutions (PETI) kuhusiana na utekelezaji wa mradi wa Amani ambapo vijana nao wanahusika katika kujenga Amani ya nchi kwa sababu wao ndio taifa la leo.
IMG_0295
Bw. Omary Hassan katika picha ya pamoja na uongozi wa taasisi ya PETI na baadhi ya wanafunzi wa taasisi hiyo.
IMG_0324
Mweka hazina wa Shirikisho la Vijana la Umoja wa Mataifa (YUNA) Tanzania Bara na Visiwani Bw. Omary Hassan akikusanya maoni kwa wananchi wa wilaya ya Karagwe kufanya tathmini ya utekelezaji wa mradi wa Amani na Demokrasia.
IMG_0378
Kina mama nao walihusika katika kuchangia maoni ambapo wengi wao wameomba mradi huo utakapoanza kuwepo na kipindi maalum katika radio jamii ya wilaya ya Karagwe cha kuwaelimisha waume zao kuhusu swala la unywaji Pombe kupita kiasi ambao unapelekea uvunjifu wa amani katika nyumba zao.
Mashirika ya UNDP na UNESCO yameanzisha mradi wa pamoja wenye lengo la kuhamasisha ushiriki wa jamii miongoni mwa vijana, wanawake na walemavu katika maendeleo na kudumisha amani nchini Tanzania.
Kama inavyojulikana haiwezekani kuwa na maendeleo bila kuwa na amani, na haiwezekani kuwa na amani bila kuwa na maendeleo.
Kwa sababu hiyo Jumuiya ya Kimataifa inatambua kuwa moja ya mikakati msingi ya kujenga amani ni kuwa na msingi thabiti wa uchumi jamii.
Pia kuwezesha raia wote kuhusisha katika kutoa maamuzi ni kuweka msimamo katika maendeleo endelevu.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU