Baadhi ya waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali nchini wakiwa
katika chumba cha mikutano cha wizara ya habari tayari kumsikiliza
Mheshimiwa waziri atangaze kamati hiyo
Mratibu wa mbio za uhuru nchini Innocent Melleck akizungumza na
waandishi wa habari juu ya mipango mbalimbali ya mbio za uhuru nchini
,Kulia ni Waziri wa habari,Vijana,utamaduni na michezo Dr Fenella
Mukangara ambapo waziri amewateuwa wajumbe kumi watakaoratibu mbio hizo
mwaka huu
Waziri wa habari,Vijana,utamaduni na michezo Dr Fenella
Mukangara akitangaza majina ya wanakamati aliowateuwa kuratibu mbio za
uhuru mwaka huu nchini
ambao amewateuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam
Kamati
hiyo inatarajiwa kuongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq na
Wajumbe wengine katika
kamati hiyo iliyoundwa na waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sofia Mjema,
Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi, Naibu Mkurugenzi wa
Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juliana Yassoda
na Mkurugenzi msaidizi Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa.
Wengine ni Mkurugenzi wa
Kampuni ya Intellectuals, Innocent Melleck, Kaimu Mhariri Mtendaji wa magazeti
ya serikali (TSN), Gabriel Nderumaki, George Kavishe kutoka Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL), Mhariri Mtendaji wa Uhuru, Jossiah Mfungo na Habib Gunze WA
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.
WAZIRI wa Habari,
Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenella Mukangara jana alitangaza wajumbe
watakaosimamia mbio za Uhuru Marathon ambazo zinatarajiwa kufanyika jijini Dar
es Salaam Desemba 8, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es Salaam jana, Dk. Fenella alisema wajumbe wa kamati hiyo
itakayokuwa na watu 10 itakuwa na jukumu la kuhakikisha mbio hizo zinafanikiwa
kwa kiasi kikubwa.
Kamati hiyo inatarajiwa
kuongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq huku ikiwa na
wajumbe wengine kutoka katika sekta mbalimbali nchini.
Wajumbe wengine katika
kamati hiyo iliyoundwa na waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sofia Mjema,
Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi, Naibu Mkurugenzi wa
Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juliana Yassoda
na Mkurugenzi msaidizi Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa.
Wengine ni Mkurugenzi wa
Kampuni ya Intellectuals, Innocent Melleck, Kaimu Mhariri Mtendaji wa magazeti
ya serikali (TSN), Gabriel Nderumaki, George Kavishe kutoka Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL), Mhariri Mtendaji wa Uhuru, Jossiah Mfungo na Habib Gunze WA
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.
Waziri Fenella alisema
mbio hizo zitakuwa zimegawanyika katika sehemu nne kukiwa na mbio ndefu za
kilomita 42, mbio za kati kilomita 21, mbio za kujifurahisha kilomita 5 na mbio
fupi ambazo ni maalumu kwa viongozi zikiwa za kilomita 3.
“Mbio hizi zina lengo kuu
la kuimarisha umoja, upendo, mshikamano na amani kwa Taifa letu. Tunategemea
Watanzania wengi, ikiwa pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, dini,
wanafunzi wa ngazi mbalimbalio na wananchi kwa ujumla wataungana na kushiriki
mbio hizi,” alisema.
Naye Mratibu wa Uhuru
Marathon, Innocent Melleck alisema wazo kubwa la kuanzisha mbio hizo ilikuwa ni
kutaka kuwakumbusha Watanzania kuuenzi umoja, amani, mshikamano ulipo pamoja na
uhuru wetu.
Mratibu huyo alisema,
mpaka sasa wanariadha zaidi ya 300 kutoka nje ya Tanzania wameomba kushiriki
mbio hizo za aina yake hapa nchini.
“Sisi kama vijana tukaona
kuna haja ya kufanya kitu cha kuwakumbusha Watanzania wenzetu kwani tunatakiwa
kudumisha urithi wa amani, mshikamano na uhuru wetu tulioachiwa na mababu
zetu,” alisema.
Melleck alisema mbali na
mbio hizo kufanyika siku hiyo, pia kutakuwa na tamasha kubwa la burudani
litakalofanyika katika Viwanja vya Leaders vilivyopo Kinondoni, Dar es Salaam
ikiwa ni mkesha wa kusubiri siku ya Uhuru.
0 maoni:
Post a Comment