Kama ni mfuatiliaji mzuri wa kipindi cha Skonga, utamkumbuka Happiness
Watimanywa, msichana pekee kutoka Tanzania aliyeweka historia ya
kuongoza nchi zaidi ya 150 za mtandao wa IGCSE katika somo la Uhasibu
kwenye mitihani ya kidato cha nne mwaka 2010.
Happy (19) ni mzaliwa wa familia ya kawaida sana ya Mr Louis Roussos ya
Morogoro. Wadogo zake Angel na Romeo sasa wanasoma St. Constantine shule
iliyomtoa Happy. Pia, Happiness Watimanywa amewahi kusoma Laureatte
International School ya Dar-es-salaam, ambapo akiwa hapo, alikutana na
mwalimu wa michezo Mr Tchalewa Ndeki ambaye alimfungulia mipaka mingi
Happy. Akiwa Laureatte, Happy aliwahi kwenda China na South Korea akiwa
na wanafunzi wenzake katika matamasha mbali mbali ya elimu na michezo.
Baada ya kumaliza kidato cha nne, Happy alifanikiwa kujiunga na Chuo
Kikuu cha Strathclyde cha UK ambapo anasomea digrii ya Biashara.
Kipindi ambacho Happy yupo kwenye likizo ndefu,
alipata wakati mgumu wa kutokuwa na kitu cha kufanya, hivyo Happy
aliamua kujihusisha na masuala ya urembo na kufanikiwa kutwaa Taji la
Miss Dodoma, na Miss Kanda ya Kati na hatimaye kuingia kwenye kambi ya
Miss Tanzania.
Akiwa Miss Tanzania, Happy alikuwa ni mshiriki wa kwanza kuingia Nusu
Fainali ya mashindano hayo kwa kutwaa taji la Redds Miss Photogenic
2013.
Ndani ya kambi ya Miss Tanzania, Happiness Watimanywa amekuwa mwiba kwa
warembo wengine 29 wanaowania taji hilo kwani amekuwa akionesha uwezo wa
hali ya juu kuanzia kwenye kipaji hata michezo, ukiachilia mbali upeo
mkubwa alio nao.
Leo ndio leo ambapo Happy anatarajia kudhihirisha
kuwa pamoja na elimu na uwezo mkubwa alio nao, pia ni mrembo. Tusubiri
matokeo ya Redds Miss Tanzania 2013.
0 maoni:
Post a Comment