Tuesday, September 3, 2013

KWA MARA YA KWANZA TANZANIA YAPATA KIKAO RASMI EALA, KIKAO KIMOJA KUFANYIKA DODOMA AU DAR

IMG_6554
Mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Afrika Mashariki, Mhe. Adam Kimbisa akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa wabunge wa Tanzania katika bunge hilo, Mh. Shy-Rose Bhanji, mbunge wa bunge hilo, Mh. Nderakindo Kessy na kulia ni Mhe. Makongoro Nyerere.
IMG_6512
Katibu wa wabunge wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania, Mh. Shy-Rose Bhanji akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mhe. Nderakindo Kessy na Mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania katika Bunge hilo, Mhe. Adam Kimbisa.
IMG_6549
Nasisitiza.....
IMG_6565
Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania wakibadilisha mawazo baada ya mkutano wao na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Katibu wa Wabunge wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania,Mh. Shy-Rose Bhanji, Mwenyekiti, Mh. Adam Kimbisa, Mh. Nderakindo Kessy na Mh. Makongoro Nyerere.
IMG_6570
Mbunge la Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania Mh. Makongoro Nyerere akipeana mkono na Katibu wa wabunge wa Tanzania katika Bunge hilo, Mhe. Shy-Rose Bhanji.
Na.Habari Mseto Blog.

Bunge la tatu EALA limeridhia Tanzania kupata kikao chake rasmi ambapo sasa kikao kitafanyika Dodoma na vikao vingine viwili kufanyika Arusha ambayo ni Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania, mhe. Adam Kimbisa amesema hayo katika mkutano na wabunge watanzania EALA, na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo.
Mhe. Kimbisa amesema katika ratiba ya vikao vya Bunge la EALA, Tanzania pia imepata rasmi kikao kimoja ambapo sasa kitafanyika mjini Dodoma.

Vile vile amesema kikao hicho kinaweza kufanyika Dar es Salaama au Zanzibar.
Amefafanua kwamba, Bunge limeridhia vikao viwili vifanyike Arusha, kimoja kifanyike Tanzania sambamba na nchi zingine wanachama; Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kupata kikao kimoja kila nchi kwa mzunguko.
Amesema nchi ambayo itakosa kikao kwa mwaka huu wa fedha 2013/2014, ndio itakuwa nchi ya kwanza kupata kikao cha mwaka ujao wa fedha.

Hata hivyo amesema, vikao vikao viwili vya Arusha vitakuwa ni vikao vya bajeti na ukaguzi wa mahesabu ambavyo ni vikao muhimu sana katika Bunge.
Mhe. Kimbisa amesema kikubwa wananchi wanachotakiwa kufahamu ni kuwa linapokuja suala la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Arusha ni Makao Makuu na kwamba haiko Tanzania kwani nchi zote tano ni wadau wa Arusha.

Naye Katibu wa watanzania,Mh. Shy-Rose Bhanji amesema ni jambo la kujivunia kwamba Tanzania sasa itakuwa na kikao rasmi kwa njia ya mazungumzo. Hii ni hatua nzuri vile wananchi pia watapata mwamko wa masuala yanayojadiliwa Bungeni.
Hatua ya maridhiano hayo imefuatia mgoghoro ulioibuka miongoni mwa wabunge wa EALA kwamba vikao vya Bunge hilo vifanyike Arusha kwa mwaka mmoja wa fedha na si kwa mzunguko kama ilivyozoeleka kuanzia Bunge la pili.

Wabunge wengi isipokuwa watanzania walitaka vikao viendelee kwa mzunguko nchini Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Arusha.

Vikao vya EALA hadi mwaka wa fedha June 2012/June 2013 vilikuwa vitano kwa mwaka. Vikao hivyo vimeongezeka kuwa sita. Vikao hufanyika kila baada ya takriban miezi miwili, kwa kipindi cha wiki mbili.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU