Kaimu Mkuu wa Huduma za Kibenki kwa kufuata
kanuni za Kiislamu (Islamic Banking) wa Benki ya NBC, Yassir Masoud (katikati)
akikabidhi mfano wa pasi ya kuingilia katika ndege ya kwenda na kurudi makka
kwa mmoja wa washindi wa promosheni ya kushinda safari ya kwenda hijja, Juma
Abdallah Kheri katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika jijini Dar es Salaam
leo. NBC itagharamia gharama zote zitakazomwezesha mshindi huyo pamoja na
mwenza wake atakayemchagua kwenda kuhiji Makka, Saudi Arabia baadae mwezi
Oktoba. Wa pili kushoto ni mke wa Juma, Sina Abdallah bwago atakayeambatana na
mumewe kwenda hijja na kulia ni Meneja Uhusiano wa NBC, Eddie Mhina.
Kaimu Mkuu wa Huduma za Kibenki kwa kufuata
kanuni za Kiislamu (Islamic Banking) wa Benki ya NBC, Yassir Masoud (kulia)
akikabidhi mfano wa pasi ya kuingilia katika ndege ya kwenda na kurudi makka
kwa mmoja wa washindi wa promosheni ya kushinda safari ya kwenda hijja, Hajra
Abdulrahman Ally katika hafla ya makabidhiano ilifanyika jijini Dar es Salaam
leo. NBC itagharamia gharama zote zitakazomwezesha mshindi huyo pamoja na
mwenza wake atakayemchagua kwenda kuhiji mjini Makka, Saudi Arabia baadae mwezi
Oktoba.
Kaimu Mkuu wa Huduma za Kibenki kwa kufuata
kanuni za Kiislamu (Islamic Banking) wa Benki ya NBC, Yassir Masoud (katikati) akizungumza
katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Meneja Uhusiano wa Benki ya NBC, Eddie Mhina
(kushoto), akimsikiliza mmoja wa washindi wawili wa promosheni ya Hijja ya
Islamic Banking ya benki hiyo, Juma Abdallah Kheri jijini Dar es Salaam leo.
0 maoni:
Post a Comment