Sunday, September 15, 2013

TIB YAZINDUA OFISI NA TAWI KANDA YA JUU KUSINI MJINI MBEYA

 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro (kulika) akikata utepe kuzindua ofisi za Makao Makuu ya Benki ya Maendelea Tanzania (TIB) ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Tawi la benki hiyo Mkoa wa Mbeya iliyofanyika jijini Mbeya jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa TIB, Peter Noni na Mwenyekiti wa Bodi ya TIB, Prof. William Lyakurwa.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo Tanzania (TIB), Prof. William Lyakurwa (kushoto), akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa ofisi za Makao Makuu ya TIB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Tawi la benki hiyo Mkoa wa Mbeya iliyofanyika jijini Mbeya. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro na Mkurugenzi Mwezeshaji wa TIB, Peter Noni.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro (katikati) akijaza fomu ili kufunguliwa akaunti ya Benki ya Maendeleo Tanzania (TIB) Tawi la Mbeya, katika hafla ya ufunguzi wa ofisi za Makao Makuu ya TIB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini pamoja na tawi hilo Mkoa wa Mbeya iliyofanyika jijini humo. wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa TIB, Peter Noni na anayeongea naye ni Mbunge wa Mbozi Masharibi, Godfrey Zambi
 Mcheza ngoma akionyesha manjonjo yake kuwaburudisha watu waliohudhuria uzinduzi huo
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro (katikati) akiagana na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo Tanzania (TIB), Peter Noni (kulia), baada ya hafla ya ufunguzi wa ofisi za Makao Makuu ya TIB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Tawi la benki hiyo Mkoani  Mbeya. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya TIB, Prof. William Lyakurwa

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU