Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) imesema uwakilishi wa ujumbe kwenye Mkutano Mkuu unaanzia
kwenye chama cha mpira wa miguu cha mkoa, kufuatiwa na chama shiriki na
baadaye klabu ya Ligi Kuu.
Mwongozo
huo juu ya uwakilishi wa wajumbe kwenye Mkutano Mkuu umetolewa kutokana
na maombi ya Sekretarieti ya TFF kwa kamati hiyo iliyokutana jana
(Septemba 16 mwaka huu) baada ya kubaini baadhi ya wajumbe wanashikilia
nafasi mbili kwenye vyama tofauti.
Kwa
mujibu wa Ibara ya 5 ya Katiba, kuna makundi ya aina tatu ya wanachama
wanaounda TFF. Makundi hayo ni vyama vya mikoa, vyama shiriki na klabu
za Ligi Kuu.
Sekretarieti
ya TFF imebaini kuwa kuna baadhi ya viongozi wa kuchaguliwa wa mikoa
ambao pia ni viongozi wa vyama shiriki na klabu za Ligi Kuu, hivyo wana
nafasi zaidi ya moja ya kuingia kwenye Mkutano Mkuu.
Hivyo,
kutokana na mwongozo huo ushiriki wa wajumbe kwenye Mkutano Mkuu wa TFF
utaanzia chama cha mkoa, kufuatiwa na chama shiriki na baadaye klabu za
Ligi Kuu.
Pia
nafasi ambazo zinaweza kuwakilishwa kwenye Mkutano Mkuu kama mhusika
hayupo ni za Mwenyekiti atakayewakilishwa na Makamu Mwenyekiti, na
Katibu atakayewakilishwa na Katibu Msaidizi. Nafasi za ujumbe wa Mkutano Mkuu na ile ya mwakilishi wa klabu hazina uwakilishi kama mhusika hayupo.
LIGI KUU YAINGIA RAUNDI YA NNE
Michuano
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia
raundi ya nne kesho (Septemba 18 mwaka huu) kwa mechi saba katika
viwanja saba tofauti.
Vinara
wa ligi hiyo, JKT Ruvu wanaonalewa na Kocha Mbwana Makata watakuwa
ugenini Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani dhidi ya Ruvu
Shooting ya Charles Boniface Mkwasa. Mechi hiyo inatarajiwa kuwa kivutio
kikubwa kwa washabiki mkoani Pwani kutokana na aina ya soka inayochezwa
na timu hizo.
Baada
ya sare dhidi ya Mbeya City wikiendi iliyopita, Yanga inaendelea kubaki
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya ambapo itacheza na
Tanzania Prisons katika mechi itakayochezeshwa na mwamuzi Simon Mbelwa
kutoka Pwani.
Nayo
Simba itaumana na Mgambo Shooting Stars ya Tanga katika mechi
itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa viingilio vya sh. 5,000,
sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Mechi hiyo itakuwa chini ya
Kamishna David Lugenge kutoka Iringa.
Uwanja
wa Kaitaba mjini Bukoba utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Oljoro JKT
kutoka Arusha na wenyeji Kagera Sugar wakati Azam na Ashanti United
zitakwaruzana kwenye uga wa Azam Complex ulioko Chamazi jijini Dar es
Salaam.
Mwamuzi
Jacob Adongo kutoka Mara ndiye atakayechezesha mechi kati ya Coastal
Union na Rhino Rangers itakayofanyika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Mtibwa Sugar inarejea uwanja wake wa Manungu ulioko Turiani mkoani
Morogoro ambapo inaikaribisha Mbeya City ya Kocha Juma Mwambusi.
Wakati
huo huo, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) nayo inaendelea kesho (Septemba 18
mwaka huu) kwa mechi moja ambapo Lipuli ya Iringa ambayo wikiendi
iliyopita ilicheza Mkamba mkoani Morogoro inapita mjini Morogoro
kuikabili Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri.
KAYUNI KUHUDHURIA KOZI YA WAKUFUNZI WA CAF.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Sunday Kayuni atashiriki warsha ya wakufunzi wa makocha wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) itakayofanyika kuanzia Oktoba 22-24 mwaka huu.
Warsha hiyo iliyoandaliwa na CAF kwa ajili ya wakufunzi wake itafanyika nchini Cameroon. Wakufunzi 18 wa CAF kwa upande wa makocha watahudhuria warsha hiyo.
Madhumuni ya warsha hiyo ni kuainisha majukumu yao, kubadilishana uzoefu. Pia kuwapa methodolojia mpya ya ufundishaji na muongozo kuhusu mfumo wa leseni za makocha ambao watautumia katika nchi wanazotoka.
Mbali ya Kayuni Tanzania, wakufunzi wengine ni Ahmed Babiker (Sudan), Amadou Shaibu (Nigeria), Boy Bizzah Mkhonta (Swaziland), Duodu Fred Osam (Ghana), Edussei Anthony (Ghana), Fathi Nossir (Misri), Faouzy Altaisha (Sudan) na Fran Hilton Smith (Afrika Kusini).
Wengine ni Francis Oti-Akenteng (Ghana), Honour Janza (Zambia), Kasimawo Laloko (Nigeria), Mahmoud Saad (Misri), Paul Hamilton (Nigeria), Serame Letsoaka (Afrika Kusini), Shawky Abdel Shafy (Misri), Thondoo Govinder (Mauritius) na Ulric Mathiot (Seychelles),

0 maoni:
Post a Comment