LEO
tungependa kupitia kwenu kutoa taarifa kuhusu maendeleo ya mradi wetu wa Uwanja wa kisasa wa mpira katika Jiji la
Jangwani kama itakavyojulikana
Mara
ya mwisho tuliongea ama kuonana ilikuwa mwezi wa tatu wakati Ndugu zetu wa BCEG
walipokabizi Concept design ama Usanifu
wa awali na kuanzia sasa tutakuwa tunatoa taarifa za mara kwa mara kuhusu
mradi huu. Wahenga walisema UKICHA KUSEMA HUTATENDA JAMBO lakini pia KUKAA
KIMYA SANA kunajenga hisia mbaya na kutoa nafasi ya upotoshwaji wa habari.
Kwa
kifupi napenda kuwakumbusha kuwa Makubalino ya Awali (Memorandum of
Understanding) yalisainiwa 23 Novemba 2012. Pamoja na mengineyo YANGA inatakiwa:
·
Kupata na kuwa na eneo la kutoshereza
malengo ya mradi
·
Kupata ushauri mzuri, michoro mizuri na
mkandarasi mzuri wa mradi
·
Kupata na kutenga fedha za kukamilisha
usanifu na ujenzi wa mradi
Kwa
upande wa BCEG wajibu wao ni kuwa na utaalamu
na uzoefu wa kutosha. BCEG wameandaa na kukabidhi michoro ya usanifu wa
awali kukidhi matakwa ya YANGA. YANGA tunatakiwa kutoa maoni yetu na na kuingia
RASMI mkataba wa ujenzi.
Kutokana na
kukua kwa Jiji la Dar es Salaam, na katika hali ya kutaka klabu iwe na vitega
uchumi klabu imeonelea ni vyema kama ingekuwa na uwanja wa mpira wa karne ya
sasa na baadaye ambao pamoja na mambo mengine utakuwa na mioundombinu
ifuatayo:-
1. Uwanja wa mpira wenye viti
40,000
2. Hostel ya wachezaji na
football academy ya vijana
3. Viwanja vya mazoezi
4. Uwanja wa kutosha kuegesha
magari
5. Hoteli na sehemu ya
makazi
6. Ukumbi wa mikutano
7. Sehemu ya maofisi, benki,
zahanati (sports clinic)
8. Maduka, supermarket na sinema
9. Sehemu za kubarizi,
kupumzikia (Recretional and Open spaces).
Mara baada ya
azma yetu kukamilika eneo hili litaitwa “Jangwani
City” na kufanya wakazi wa maeneo ya Jangwani na sehemu za jirani wasiende
maeneo ya mbali kutafuta huduma muhimu za kijamii. Eneo hili litaboresha mandhari
nzima ya Jangwani kwa kukuza mazingira na miundombinu. Hii itahusu pamoja na
mambo mengine ujazaji udongo (tuta kubwa), upandaji miti, bustani za kubarizi,
kuboresha mifereji ya majitaka na kudhibiti mafuriko ya eneo la Jangwani na hivyo kulipatia sura ya kibiashara na kitalii.
Ili kukamilisha
azma ya kuwa na Jangwani City itakayo kuwa na miundombinu yote hiyo, Uongozi
ulipeleka maombi ya eneo la nyongeza Manispaa
ya Ilala na Wizara ya Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi kwa barua zenye kumbukumbu namba
YASC/ARDHI/MWK/YM/46/2012 na YASC/ARDHI/MWK/YM/47/2012 za 12 Desemba 2012, na
mpaka sasa bado maombi yetu hayajajibiwa.
Mwezi wa saba,
Wadhamini/Uongozi wa YANGA walimwandikia Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam kuomba msaada wake kufanikisha maombi ya nyongeza ya kiwanja yaliyowasilishwa
Manispaa ya Ilala na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Klabu ya Yanga
ina kiwanja chenye ukubwa wa hekta 3.59 eneo la Jangwani. Kiwanja hiki kina
hati miliki kwa miaka 99 toka mwaka 1972 na katika eneo hilo, klabu ilifanikiwa
kujenga uwanja wa mpira wa Kaunda na Jengo la klabu la ghorofa tatu. Jengo hili
lilijengwa kwa ufadhili mkubwa sana wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee
Abeid Amani Karume (Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi) na michango ya
wanachama na wapenzi wa klabu ambao kila siku wamekuwa wakiamini kuwa haba na
haba hujaza kibaba.
Ndugu Wandishi
wa habari kwa kifupi tumefikia hapo, zoezi la kutoa maoni yetu kuhusu michoro
ya usanifu wa awali na kuingia rasmi mkataba wa ujenzi na BCEG limesimama,
likisubiri majibu ya nyongeza la eneo. Ni matumaini yetu zoezi hili litakamilika hivi
karibuni na kuendelea na mradi.
0 maoni:
Post a Comment