Biashara ya samaki kwenye Mwalo wa Musoma mkoani Mara na Kirumba mkoani Mwanza imepata msukumo wa kipekee baada ya kuanzishwa kwa kampeni ya hakatwi mtu, ambayo inawawezesha watumiaji wa mtandao wa airtel kutuma na kupokea pesa bila makato.
Ikiwa inaingia katika mwezi wa tatu sasa kampeni ya hakatwi mtu inayowawezesha wateja wa airtel money kufanya miamala yao bila makato, wafanyabiashara na wachuuzi kwenye soko la samaki la Mara Mmusoma
wanatumia kampeni hiyo kama njia ya kupunguza kutembea na pesa muda wote kwa ajili ya kununua ama kuuza samaki na dagaa
mwenyekiti wa soko la samaki na dagaa mwaloni Musoma Mara bw, Gideon Dogori anasema airtel money hakatwi mtu ni sawa na kufanya biashara ya malipo kamili yaani cash kutokana na falsafa yake ya hakatwi mtu.
Anasema wafanyabiashara sokoni hapo hufanya malipo kwa kutumia airtel money na hawana tena ulazima wa kutembea na maburungutu ya fedha kwa ajili ya kununulia dagaa ama samaki.
"Tangia hawa jamaa wa airtel waanzishe hii huduma yao ya hakatwi mtu wafanyabiashara hapa wamekua hawatembei na lundo la hela kama ilivyokua mwanzoni bali sasa wanauza na kununua bidhaa kwa kutumia
simu zao za mkononi",alisema Bw. Dogori.
"Kuna wengine wanaishi nje ya Musoma kwahiyo wanatuma tu pesa na wanatumiwa bidhaa zao huko walipo bila kufika hapa sokoni kwasababu huduma ya airtel money haina makato yoyote" aliendelea kueleza
mwenyekiti wa mwalo wa samaki na dagaa musoma bw. Dogoli.
Bw Dogori anasema faida kubwa inaonekana kwenye huduma hii hasa kuokoa muda kwa wafanyabiashara, ambapo hawahitajiki kusafiri mwendo mrefu kwenda sokoni hapo kufanya manunuzi kama ilivyokuwa zamani bali wanatuma tu hela na kusubiria bidhaa zao huko walipo.
"Huduma hii ingekuwa ya kudumu ingesaidia sana wafanyabiashara kwani ka muda huu mfupi imeweza kusaidia kuongeza hata miataji kwa wafanaybiashara hapa mwaloni", alisisitiz Dogori.
Bi Mkami Magesa ni mfanyabiashara kwa zaidi ya miaka kumi sokoni hapo, anasema wakati huu biashara imerahisishwa sana kwani kupitia huduma ya hakatwi mtu amekuwa akifanyabiashara kubwa na anapata pesa yake bila makato.
"Hii huduma ya airtel money ya hakatwi mtu ni mkombozi kwakweli kwani mteja anaweza akawa shinyanga ama singida anatuma humu pesa na mimi nampakilia mzigo wake anaupata bila ya yeye kufika hapa mwalini",
alisema bi Mkami.
Kwa upande wake John Anton mchuuzi wa dagaa na samaki katika soko la samaki Mwaloni Mwanza Anasema anachofanya ni kutoa oda ya bidhaa anazohitaji na kisha kutuma pesa bila makato kwenda kwa muuzaji na kuokoa muda wa kusafiri kutoka sirali anapoishi na kufanyia biashara zake.
"Kwasasa maisha na biashara imekuwa rahisi sana nawaomba airtel kuifanay huduma hii kuwa endelevu maana inasaidia sana katika shughuli za kibiashara", alisema Bw. Bundala.
Bw Dogori ambaye ni mwenyekiti wa mwaloni mjini Musoma alimalizia kwa kusema elimu zaidi ya matumizi ya huduma za airtel money inahitajika kwani zimeanza kuonesha dalili za kuwa mkombozi kwa wafanyabiashara wa soko lake.
0 maoni:
Post a Comment