Sunday, October 6, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT.BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA 6 LA KIMATAIFA LA MADAKTARI WANANFUNZI, JIJINI MWANZA LEO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano la Sita la Kimataifa la Madktari Wanafunzi, lililofanyika sambamba na Mkutano wa nne wa Chama cha Madaktari Wanafunzi TAnzania (TAMSA) lililofanyika jijini Mwanza leo, Oktoba 6, 2013.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Afya, Dkt. Hussein Mwinyi (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Eng. Evarist Ndikilo, wakijumuika kuimba wimbo wa Taifa kabla ya kufunguliwa kwa Kongamano hilo.
 Baadhi ya wananfunzi Madaktari, wakijumuika kuimba wimbo wa Taifa, kabla ya kuanza kwa Kongamano hilo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea Cheti kutoka kwa Mratibu wa Kongamano la Sita la Kimataifa la Madktari Wanafunzi, lililofanyika sambamba na Mkutano wa nne wa Chama cha Madaktari Wanafunzi TAnzania (TAMSA) ambaye ni mwanafunzi wa Chuo cha Hubat Kairuki cha Dar es Salaam, Helga Mutasingwa, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa Mhe. Makamu katika kufanikisha Kongamano hilo. Makamu alipokea Cheti hicho leo Oktoba 6, 2013 baada ya kufungua rasmi Kongamano hilo jijini Mwanza. Picha na OMR
 Sehemu ya Wanafunzi, Madaktari waliohudhuria Kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais wakati alipokuwa akisoma hotuba yake ya ufunguzi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi Madaktari, baada ya ufunguzi rasmi wa Kongamano hilo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Anthony Dialo, na baadhi ya viongozi baada ya kufungua Kongamano hilo, jijini Mwanza leo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya wanafunzi Madaktari baada ya kufungua Kongamano hilo, jijini Mwanza leo. Picha na OMR

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU