Rais Kikwete akikaribishwa kutembelea Jengo
la Bunge mjini Dodoma na Naibu Spika Mhe. Job Ndugai leo Oktoba 24, 2013
Rais Kikwete akiangalia sehemu ya viti ndani
ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo
Oktoba 24, 2013
Rais Kikwete akitembelea Ukumbi wa Bunge mjini
Dodoma leo Oktoba 24, 2013
Rais Kikwete akisindikizwa na Naibu Spika
Mhe Job Ndugai na Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashilila baada ya kutembelea Ukumbi
wa Bunge mjini Dodoma leo Oktoba 24, 2013
Rais Kikwete akizungumza na Naibu Spika Mhe
Job Ndugai na Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashilila baada ya kutembeleaUkumbi wa
Bunge mjini Dodoma leo Oktoba 24, 2013
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete leo, Alhamisi, Oktoba 24, 2013 ametembelea na kukagua Jengo la Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania mjini Dodoma kujionea maandalizi ya jinsi Wabunge wa Bunge
Maalum la Katiba watakavyokaa katika Ukumbi wa Bunge hilo. Bunge hilo Maalum la
Katiba litakuwa na Wabunge 600 tofauti ya Bunge la sasa lenye Wabunge 354 ambao
ni pamoja na Wabunge 239 wa kuchaguliwa kutoka majimboni, Wabunge Wanawake Viti
Maalumu 102, Wabunge wa kuteuliwa toka Baraza la Wawakilishi Zanzibar 5, Mwanasheria
Mkuu wa Serikali na Wabunge 7 (kati ya 10) wa kuteuliwa na Rais.
0 maoni:
Post a Comment