Tuesday, November 19, 2013

AIRTEL YAZINDUA PROMOSHENI YA MIMI BINGWA

 Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Bw. Sunil Colaso akielezea jinsi Airtel inavyowathamini wateja wake kwa kuwawezesha kushinda tiketi za kuweza kujionea mechi mojawapo ya Timu ya Manchester United

 Baadhi ya wadau mbalimbali wakifuatilia kwa umakini uzinduzi wa promosheni hiyo mpya ya ‘MIMI NI BINGWA’ uliofanywa na Airtel Tanzania kwa ushirikiano na klabu ya Manchester United
 Meneja Uhusiano wa Timu ya Manchester United, Bw. Michael Higham akielezea faida za muungano kati ya Airtel Tanania na  Manchester kuwa utaongeza hata idadi ya mashabiki wa klabu hiyo kwa Watanzania.
 Mkurugenzi wa Kitengo cha Masoko kutoka Airtel Tanzania, Bw. Levi Nyakundi (kushoto) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Kitengo cha Masuala ya Fedha Airtel Tanzania, Bw. Kalpesh Mehta wakifuatilia kwa umakini kabisa uzinduzi wa promosheni hiyo mpya.

Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde ambaye alikuwa ni mshehereshaji wa uzinduzi wa promosheni ya ‘MIMI NI BINGWA’ akizungumzia promosheni mpya ya Airtel iliyozinduliwa jana katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam. Kutoka kulia ni Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo,  Bw. Leornad Thadeo, Mkurugenzi wa Airtel Tanzania  Sunil Colaso pamoja na Meneja Uhusiano wa Timu ya Manchester United, Bw. Michael Higham. 
 

Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Bw. Sunil Colaso akimkabidhi jezi ya Timu ya Manchester United Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bwana Leornad Thadeo jezi mpya ya  Manchester United.
 

Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Bw. Sunil Colaso akimkabidhi jezi ya Timu ya Manchester United, raisi mpya wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania Bw. Jamal Malinzi
 
 Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso akimkabidhi jezi ya Timu ya Manchester United mtangazaji wa Clouds FM, Bw. Ephraim Kibonde ambaye alichukua kwa niaba ya wapenzi wa mpira.
Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Bw. Sunil Colaso (wa pili kutoka kushoto) akiwa pamoja na Meneja Uhusiano wa Timu ya Manchester United, Bw. Michael Higham  (wa kwanza kushoto). Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Bw.  Leornad Thadeo, Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na  Mtangazaji wa Clouds FM, Bw. Ephraim Kibonde muda mfupi baada ya uzinduzi wa promosheni ya ‘MIMI NI BINGWA’ iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU