Tuesday, November 26, 2013

BALIMI MUSOMA

Displaying WASHINDI WA KWANZA NYARUSURYA GROUP WA KISHANGILIA.JPG 
Kikundi cha Nyarusurya wakishangilia mara baada ya kuongoza wenzao na kutwaa ubingwa katika mbio za mitumbwi zilizofanyika mwishoni mwa wiki Musoma.Picha na Mpiga Picha Wetu.
 
KIKUNDI cha Nyarusurya Group cha wapiga kasia Wanaume kutoka Musoma Mjini,kimetwaa ubingwa wa mashindano ya mbio za Mitumbwi zinazodhaminiwa na Kampuni ya Bia nchini kupitia Bia ya Balimi Extra Lager na hivyo kujitwalia zawadi ya fedha taslimu Shilingi 900,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa wa Mara katika mashindano ya Kanda yanayotarajiwa kufanyika jijini Mwanza hivi karibuni.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na kikundi cha nahodha Bernard toka kinesi ambao walizawadiwa fedha taslimu shilingi 700,000/= pamoja na nafasi ya kuwakilisha mkoa huo pia katika fainali za Kanda pale jijini Mwanza ,nafasi ya tatu ilichukuliwa na kikundi cha nahodha Benedkito Chamba kutoka Bwai ambao walizwadiwa fedha taslimu shilingi 500,000/= , nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha Mweme kutok a Kinesi ambao walijinyakulia zawadi ya fedha taslimu shilingi 400,000/= na nafasi ya sita mpaka ya kumi walipewa kufuta jasho cha fedha taslimu shilingi 250,000/= kwa kila kikundi.

Upande wa Wanawake kikundi cha Kisorya Group kutoka Kisorya Bunda ambao walikuwa mabingwa wa kanda mwaka jana upande wa wanawake,Kilitwaa ubingwa na hivyo kuzawadaiwa fedha taslimu Shilingi 700,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa wa Mara,kwenye mashindano ya Kanda pale jijini Mwanza mwezi ujao.

Nafasi ya pili upande wa wanawake ilichukuliwa na kikundi cha Nyamiti kutoka Majita ambao walijinyakuliwa zawadi ya fedha taslimu shilingi 600,000/= pamoja na kuwakilisha mkoa huo kwenye fainali za Kanda upande wa Wanawake pale jijini Mwanza,nafasil ya tatu ilichukuliwa na kikundi cha Mama Lameck Kutoka Lukuba ambao walizawadiwa fedha taslimu shilingi 400,000/=,nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi chaRhob kutoka Kinesi, ambao walijinyakulia zawadi ya fedha taslimu shilingi 300,000/= nafasi ya sita mpaka ya kumi walipewa kifuta jasho ya fedha taslimu cha shilingi 200,000/= kila kikundi.

Akizungumza mgeni rasmi wa mashindano hayo Ambaye ni mkuu wa upelelezi wilaya ya Musoma,Juma Mataka wakati wa kukabidhi zawadi Mbali mbali kwa washindi wa shindano hilo alisema kuwa Kampuni ya Bia Tanzania kwa kutambua umuhimu wa Mashindano Hayo kupitia bia yake ya Balimi wameamua kuboresha mashindano ya kupiga kasia ili kuwawezesha washiliki kujiingizia kipato.

Nae Mwakilishi wa Tbl meneja  mauzo wa kanda ya ziwa, Malaki Sitaki alisema kuwa Kampuni ya Bia Tanzania imeamua kutengeza ajira kupitia  mashindano ya Kupiga kasia ili kuwawezesha wavuvi kujiingiza kipato na kuweza kuheshimika kutokana na ajira hiyo kuwa imetupwa na watu wengi kutokana na wahusika kuonekana  katika jamii kuwa ni watu walioshindwa maisha.

Fainali za Kanda za mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika Decemba 7,2013, katika ufukwe wa Mwaloni jijini Mwanza ambapo watashindana mabingwa wa Kanda nzima toka mikoa ya Kigoma, Kagera,Ukerewe,Musoma na wenyeji Mwanza.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU