Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu
(kushoto), akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya
Umma (PPF) William Erio katika hafla iliyoandaliwa na bodi kwa wateja wa
makampuni kubadilishana mawazo na kuwajulisha mipango na maendeleo ya benki hiyo.
Wa pili kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sekta za Umma na Huduma za Kibenki kwa
Taasisi wa benki hiyo, William Makoresho na kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mauzo
Hazina, Burton Hamisi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NBC, Dk. Mussa
Assad (kulia) akisalimiana na mmoja wa wateja wa makampuni ya benki hiyo, Ankush
Shah katika hafla hiyo. Katikati ni Mujumbe wa Bodi ya NBC, Daniel Btits.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Bi. Mizinga Melu
(kulia), Mjumbe wa Bodi, Dk. Hussein Kassim (kushoto), wakifurahi pamoja na
baadhi ya wateja wa benki hiyo katika hafla hiyo ambayo NMBC imesema huo ni
mwanzo wa matukio ya kila mara ambapo viongozi watakuwa watakutana na wateja
ili kujua mahitaji yao na kubadilishana mawazo.
Wa pili kushoto ni Rishad Karimjee na Farishta Kohli wote kutoka Toyota.
Mkurugenzi Mkuu
wa Mfuko wa Akiba wa Mashirika ya Umma (PPF), William Erio (katikati) akisalimiana
na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki kwa Wateja Wakubwa cha Benki ya NBC
Tanzania, Andre Potgieter katika hafla. Kushoto ni Naibu Mkuu wa Kitengo cha
Wateja Wakubwa wa NBC, Minnie Adolf Kibuta.
Baadhi ya wateja wakibadilishana mawazo na maofisa wa
NBC katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam.
0 maoni:
Post a Comment