Sunday, November 3, 2013

BONIFACE WAMBURA AULA TFF AWA KAIMU KATIBU MKUU WA TFF

KAIMU KATIBU MKUU WA TFF BONIFACE WAMBURA.
 
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemteua Bw. Boniface Wambura kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF. Uteuzi huo ni kuanzia Novemba 2 mwaka huu.

Aidha aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah ameagizwa aende likizo ya malipo hadi atakapomaliza mkataba wake.

Kamati ya Utendaji inaviomba vilabu, vyama vya wilaya, vyama vya mikoa, vyama shiriki na wadau wote kumpa ushirikiano Bw. Boniface Wambura katika utekelezaji wa majukumu yake.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU