Usajili wa wachezaji kwa dirisha dogo
kwa msimu wa 2013/2014 Tanzania Bara unafunguliwa Novemba 15 mwaka huu na
utafungwa rasmi Desemba 15 mwaka huu.
Kwa mujibu wa kanuni, klabu zenye fursa
ya kusajili wachezaji katika dirisha dogo ni zile ambazo hazijatumia nafasi
zote 30 za wachezaji.
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja
la Kwanza (FDL) zimemaliza duru la kwanza msimu huu. Duru za pili litaanza
kutimua vumbi Januari mwakani.
Kwa mujibu wa Kalenda ya Matukio ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) matukio ya Novemba na Desemba ni
dirisha dogo la usajili na mechi za kirafiki za Shirikisho la Kimataifa la
Mpira wa Miguu (FIFA)- FIFA Date.
Matukio mengine ni michuano ya Kombe la
Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 wa klabu za VPL na
michuano ya Kombe la Chalenji itakayofanyika Nairobi, Kenya.
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 maoni:
Post a Comment