Monday, November 4, 2013

MAKINDA AONGOZA USAJILI WA MARATHON

USAJILI wa mbio za Uhuru Marathon, unatarajiwa kuanza kutingisha wengi wakati Spika wa Bunge, Anne Makinda leo katika Viwanja vya Bunge, anatarajiwa kuwaongoza wabunge mbalimbali kujisajili kwa ajii ya kushiriki mbio hizo.

Katibu wa Kamati ya Uhuru Marathon, Innocent Melleck alisema, Makinda anatarajiwa kujisajili ili kushawishi wabunge wengi kushiriki mbio hizo ambazo lengo lake kubwa ni kusisitizia umoja, amani na mshikamano uliopo miongoni mwa Watanzania.

Melleck alifafanua kuwa, fomu hizo zitatolewa kwa Sh 100,000 kwa wale watakaokimbia mbio za kilomita tatu, Sh 2,000 mbio za kilomita tano, Sh 6,000 kwa atakayeshiriki moja kati ya mbio za kilomita 21 au 42.

“Hizi mbio ni muhimu zaidi kwa ajili ya Taifa letu, hivyo ni vyema kwa Watanzania wote wakashiriki ili kuipigania amani iliyopo nchini mwetu na ndiyo maana hata Rais Jakaya Kikwete, pia atashiriki.

“Kesho (leo) Spika Makinda anatarajiwa kuwaongoza pia wabunge wanaotaka kushiriki mbio hizo na ni imani yetu wajitokeza kwa wingfi kushiriki,” alisema.

Mratibu huyo alisema mbio za kilomita 3 zitakuwa maalumu kwa ajili ya viongozi wa kada mbalimbali, wakiwemo pia wale wa dini na zile za kilomita 5 pia zitakuwa za kuchangia kwa ajili ya watu wa mahitaji maalumu.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU