Meneja wa
Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akiwasha trekta wakati wa hafla fupi ya
kumkabidhi mjasiliamali wa kilimo, Filemon Choroha(chini kushoto) aliyefaulu
kupewa kifaa hicho katika awamu ya pili ya program ya Wezeshwa na Safari Lager.Hafla
ya makabidhiano ilifanyika Dar es Salaam jana.
Meneja wa
Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo(kulia) akimkabidhi mjasiliamali, Filemon
Choroha kadi ya Trekta na funguo, ikiwa ni ruzuku ya program Wezeshwa na
Saafari Lagar awamu ya pili ambapo mjasilamali huyo alifuzu kupewa. Hafla ya
makabidhiano ilifanyika Dar es Salaam jana.
Meneja wa
Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo(kulia) akimkabidhi mjasiliamali, Filemon
Choroha kadi ya Trekta na funguo, ikiwa ni ruzuku ya program Wezeshwa na
Saafari Lagar awamu ya pili ambapo mjasilamali huyo alifuzu kupewa. Hafla ya
makabidhiano ilifanyika Dar es Salaam jana.Kushoto ni Jaji Mkuu wa Taasisi ya
TABDS, Joseph Migunda, kutoka kampuni ya TABDS.
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar
Shelukindo(kulia) akimkabidhi mjasiliamali, Filemon Choroha Trekta baada ya
kufuzu vigezo katika awamu ya pili ya program ya Wezesha na Safari Lager. Hafla
ya makabidhiano ilifanyika Dar es Salaam jana.
Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imekabidhi rasmi
Tractor mpya kabisa aina ya SOLANIKA
DI-75 RX kwa mjasiriamali Filemoni Choroha wa mkoani Morogoro. Makabidhiano
haya yamefanyika chini ya programu ya “Safari
Lager Wezeshwa”.
Akizungumza katika hafla fupi ya
kukabidhi Tractor hiyo jijini Dar Es Salaam leo Meneja wa bia ya Safari Lager
Bw. Oscar Shelukindo alifafanua kwamba hii ni ruzuku ya mwisho kugaiwa kwa
wajasiriamali baada ya makabidhiano mengine ya ruzuku kwa wajasiriamali
yaliyofanyika katikati ya mwaka huu katika mikoa ya Arusha, Mwanza Mbeya na Dar
Es Salaam.
Bw. Oscar alifafanua namna washindi
walivyopatikana, ngazi ya kwanza ya programu hii ilihusisha wajasiriamali
wadogowadogo kujaza kwa usahihi na kutuma fomu za maombi ya ruzuku. “Tunawashukuru
watanzania wote kwani kulikuwa na maombi kutoka mikoa mingi sana ya Tanzania, jumla
ya mikoa 23 ilishiriki zoezi hili. Hii inaonyesha wajasiriamali wa Tanzania
wana muamko wa kujiendeleza na kuendeleza jamii inayowazunguka, kuwasaidia
kutimiza ndoto hii ndio lengo kuu la shindano hili.”
Bw. Shelukindo alifafanua kwamba
baada ya fomu za maombi ya ruzuku kukusanywa zilichambuliwa na majaji wenye
utaalamu wa mambo ya biashara. Jumla ya fomu 11,230 zilikusanywa ambapo wajasiriamali
68 walichaguliwa. Timu ya wataalamu hawa wa biashara waliwatembelea
wajasiriamali waliochaguliwa ili kuhakiki uwepo wa biashara zao na ndipo
wajasiriamali 46 wakachaguliwa kupata ruzuku za mpango huu wa “Safari Lager Wezeshwa”. Ili kufikia
wajasiriamali wengi kwa ukaribu zaidi, mikoa ilitengwa katika kanda nne,
mafunzo na ruzuku zilikabidhiwa kwa wajasiriamali katika kanda hizi badala ya
wote kukusanyika katika mkoa mmoja. Jumla ya ruzuku ya thamani ya shilingi
milioni mia mbili zimegawanywa kwa wajasiriamali waliofaulu programu hii katika
msimu wa pili.
Bwana Shelukindo aliendelea kusema,
“Ili kutoa changamoto kwa wajasiriliamali hawa watumie ruzuku zao vizuri,
Safari Lager tumeona tusiwatupe mara baada ya kuwapatia ruzuku. Wataalamu wamewatembelea
mara kwa mara ili kuwasaidia walipokwama. Kwa mwaka huu tumetoa ruzuku nyingine
zaidi kwa wajasiriamali waliofanya vizuri msimu uliopita”. Aliwataja
wajasiriamali hao kwamba ni, Bibie Msumi, Benedict Matandiko, Vumilia Mtweve,
Gregory Kiria, Johnson F. Mrema na Lilian Sandu Moshi.
Akizungumzia ushiriki wa wajasiriamali katika zoezi hili jaji
mkuu Bw. Joseph Migunda wa taasisi ya TAPBDS alisema wajasiriamali wa rika zote
walijitokeza, idadi ya wanaume walioshiriki ni asilimia 62 ya washiriki wote,
na wanawake ni asilimia 38. Alisema pia maombi yalitoka katika fani nyingi
sana, mafundi wa aina mbalimbali kama magari, nguo na kuchonga samani za ndani,
watoa huduma kama hoteli, mitandao ya mawasiliano, wazalishaji kama wa vyakula
vya kusindika, kukoboa nafaka nk wote wamejitokeza kuomba kuwezeswa na Safari
Lager. Alisema vigezo vilivyotumika ni mtu awe na biashara yake mwenyewe,
mchapakazi na mwenye lengo la kujiendeleza na kusaidia jamii inayomzunguka.
Majaji waliangalia ubunifu wa wazo la biashara, uwezo wa kujieleza na kama fomu
imejazwa vizuri na ina viambatanishi vyote. Asilimia 28 ya fomu zote
hazikujazwa kwa usahihi.
Bwana Shelukindo alimaliza kwa
kuwashukuru watanzania wote kwa ushiriki huu, na aliwaomba radhi wajasiriamali
ambao bado wanaendelea kutuma na ambao bado wako na fomu kwamba muda wa
kurudisha umekwisha, aliwaomba watege sikio katika vyombo vya habari na
watataarifiwa muda mwingine wa kutuma maombi ya Programu ya “Safari Lager Wezeshwa.”
0 maoni:
Post a Comment